Teua Kazi/Hali kwenye paneli dhibiti ili uonyeshe menyu ya Kazi/Hali. Unaweza kukagua hali kichapishi au kazi.

|
|
Hubadili orodha zilizoonyeshwa. |
|
|
Chuja kazi kwa utendaji. |
|
|
Wakati Inatumika imeteuliwa, huonyesha orodha ya kazi zinazoendelea na kazi zinazosubiri kuchakatwa. Wakati Kumbukumbu imeteuliwa, huonyesha historia ya kazi. Unaweza kukatisha kazi au kukagua msimbo wa kosa ulioonyeshwa kwenye historia wakati kazi imeshindikana. |
|
|
Huonyesha makosa yoyote ambayo yametokea kwenye kichapishi. Teua kosa kutoka kwenye orodha ili kuonyesha ujumbe wa kosa. |
|
|
Hubadili orodha zilizoonyeshwa. Unapotumia nafasi ya ziada ya kioleosura, unaweza kunadilisha vichupo ili kuonyesha hali ya kipengee cha hiari. Tazama maelezo husiani kwa maelezo zaidi. |
|
|
Huonyesha makadirio ya kiwango cha wino na kiwango cha maisha ya huduma ya kikasha cha ukarabati. |
|
|
Inaonyesha makadirio ya matumizi ya nishati. Kiwango cha nishati kilichoonyeshwa ni thamani ya mwongozo wa matumizi ya jumla na kinaweza kuwa tofauti kutegemea unavyotumia kipengee hiki. Kinahesabiwa kwa kutumia fomula inayofuata. <Kiwango cha nishati kinachohitajika kuchapisha kwenye ukurasa moja wa karatasi * kwa bidhaa hii>×<Idadi ya kurasa zilizochapishwa katika siku 7 zilizopita> Tazama ufafanuzi unaofuata kwa maelezo kuhusu matumizi ya nishati ya bidhaa fulani. * Data iliyotumika kuchapisha ukurasa moja wa karatasi ndiyo data ya kipimo cha kiwango cha TEC ya ISO / IEC10561 1999 ya muundo wa kipimo cha A. Kuhusu matumizi ya nishati ya bidhaa fulani Thamani ya TEC*1 ya bidhaa hii ni takriban 1/3 ya thamani ya kawaida*2 ya kuunganisha Programu ya Nyota ya Nishati ya Kimataifa. |
*1 TEC ni kifupisho cha matumizi ya Umeme Kawaida na ndiyo matumizi ya nishati (kWh) kwa wiki kamili (siku 5 za uendeshaji uliorudiwa na kulala / kuzima + siku 2 za kulala / kuzima). Kiwango hiki kinatumika kama kiwango cha marejeleo kufuata “Programu ya Kimataifa ya Nyota ya Nishati”. Tazama tovuti ya Epson au uwasiliane na usaidizi wa Epson ili kupata thamani ya TEC ya bidhaa hii.
*2 Viwango kamili vya kuendana na Programu ya Kimataifa ya Nyota ya Nishati vimewekwa ili 25% bora ya bidhaa zenye utendaji bora wa kuhifadhi nishati kuendana na kiwango hiki.