Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Chaguo Msingi za Menyu kwa Kunakjili
Hali ya Rangi
Teua iwapo utatambaza kwenye rangi au katika rangi moja.
Otomatiki
Hutambua iwapo nakala asili ni ya rangi au monokromu, na hunakili kiotomatiki kwa kutumia modi ya rangi inayofaa zaidi.
Kulingana na nakala asili, nakala asili za monokromu zinaweza kutambuliwa kama za rangi, au nakala asili za rangi kama monokromu. Iwapo utambuzi otomatiki haufanyikazi sahihi, nakili kwa kuteua Rangi au Ny'i na Ny'pe kama modi ya rangi, au kuweka unyeti wa utambuzi. Unaweza kuweka unyeti kwa kuteua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani > Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao > Nakili Kiwango Hisi cha Rangi.
Rangi
Hunakili nakala asili katika rangi.
Ny'i na Ny'pe
Hunakili nakala asili katika rangi nyeusi na nyeupe (rangi moja).
Uzito
Ongeza kiwango cha uzito wakati matokeo ya kunakili yamefifia. Punguza kiwango cha uzito wino unapomwagika.
Mipangilio ya K'si
Chagua chanzo cha karatasi ambacho unataka kutumia. Wakati Otomatiki imeteuliwa, ukubwa unaofaa unaingizwa kitomatiki kulingana na ukubwa halisi uliogunduliwa kiotomatiki na uwiano wa ukuzaji uliobainishwa.
Punguza/Ongeza
Husanidi mgao wa ukuzaji wa upanuaji au upunguzaji. Donoa thamani na ubainishe ukuzaji unaotumika kuongeza au kupunguza nakala asili ndani ya masafa ya 25 hadi 400%.
Otomatiki
Hutambua eneo la kuchapisha na kukuza kiotomatiki au kupunguza nakala asili ili itoshee kwenye ukubwa wa karatasi uliyoteua. Wakati kuna pambizo nyeupe kwenye nakala asili, pambizo hizo nyeupe kutoka kwenye alama () ya kona ya kioo cha kitambazaji zinatambuliwa kama eneo la kutambaza, lakini pambizo katika upande mkabala zinaweza kupunwa.
Pu. ili Itoshee Kar'i
Hunakili picha zilizotambazwa kwa ukubwa mdogo kuliko thamani ya Punguza/Ongeza ili kutoshea ndani ya ukubwa wa karatasi. Iwapo thamani ya Punguza/Ongeza ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi, huenda data ikachapishwa zaidi ya kingo za karatasi.
Fomu Wazi(mm)
Bainisha urefu wima na mlalo wa karatasi ili uipanue au upunguze.
Fomu Wazi(%)
Bainisha vikuzaji tofauti vya urefu wima na mlalo wa nakala asili ili kuikuza au kuipunguza.
Saizi Halisi
Hunakili kwa ukuzaji wa 100%.
A4→A5 na nyingine
Hukuza au kupunguza nakala asili kiotomatiki ili kutoshea kwenye ukubwa wa karatasi bainifu.
Aina Asili
Teua aina ya nakala yako asili. Hunakili katika ubora wa juu ili kulingana na aina ya hati halisi.
Pande 2
Teua muundo wa pande 2.
1→Upande 1
Hunakili upande mmoja wa hati halisi kwenye karatasi ya upande moja.
2>Pande 2
Hunakili pande zote za hati halisi kwenye pande mbele ya karatasi moja. Teua mwelekeo wa nakala asili na eneo la kuunganisha nakala asili na karatasi.
1>Pande 2
Hunakili hati halisi zenye pande mbele kwenye pande mbili za karatasi moja. Teua mwelekeo wa nakala asili na eneo la kuunganisha karatasi.
2>Pande 1
Hunakili pande zote za hati halisi kwenye upande mmoja wa karatasi moja. Teua mwelekeo wa nakala yako asili na nafasi ya muunganisho ya nakala asili.
Kurasa Nyingi
Teua muundo wa nakala.
Ukurasa Mmoja
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.
2-juu
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.
4-juu
Hunakili hati halisi zenye pande nne kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 4-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.
Kumalizia
Teua jinsi ya kuondoa karatasi kwa nakala anuwai za hati halisi anuwai.
Kikundi (Kurasa Sawa)
Hunakili nakala asili kwa ukurasa kama kikundi.
Pangiliza (Mpang'o wa Ukurasa)
Huchapisha nakala nyingi za hati nyingi halisi zilizolinganishwa kimpangilio na kupangwa kwenye vikundi.