Kuchapisha Ripoti ya Muunganisho wa Mtandao

Unaweza kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili kuangalia hali kati ya kichapishi na kipanga njia pasiwaya.

Iwapo unataka kusanidi mipangilio kwenye kichapishi kilichowezeshwa kwa Mpangilio wa Kufunga, ni lazima uingie kama msimamizi.

Ikiwa imeonyeshwa kwenye skrini ya kichapishi, gusa ikoni hii na uingie kama msimamizi.

  1. Teua Mipangilio kwenye skrini ya mwanzo.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Ukaguzi wa Muunganisho.

    Ukaguzi wa muunganisho unaanza.

    Kumbuka:

    Unapotumia mtandao wa ziada, menyu ya kusanidi orodha ya mipangilio ya mtandao imegawanywa katika kiwango kawaida na ziada kwa hatua zilizo hapa juu. Tazama maelezo husiani kwa maelezo zaidi.

  3. Fuata maagizo wakati matokeo ya utambuzi tatizo yanaonyeshwa kwenye skrini.

    Iwapo kosa limetokea, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao na kisha ufuate masuluhisho yaliyochapishwa.