Unaweza kutafuta Kikasha pokezi/Siri kwenye Kasha la Faksi kwenye skrini ya nyumbani.
Kikasha pokezi/Siri
Kisanduku pokezi na Vikasha vya Siri(Orodha)
Kisanduku pokezi na vikasha vya siri kwenye Kasha la Faksi > Kikasha pokezi/Siri.
Unaweza kuhifadhi hadi nyaraka 200 kwenye kikasha pokezi na kikasha cha siri kwa jumla.
Unaweza kutumia Kikasha pokezi kimoja na usajili hadi vikasha 10 vya siri. Jina la kikasha linaonyeshwa kwenye kikasha. Ya siri XX ni jina chaguo-msingi kwa kila kikasha cha siri.
Kisanduku pokezi na Vikasha vya Siri
Huonyesha orodha ya faksi zilizopokewa kwa jina la mtumiaji, tarehe zilipokelewa na kurasa. Iwapo Jina la Faili limewekwa kwenye Nyingine, jina la faili huonyeshwa badala ya jina la mtumaji.
Uhakiki
Huonyesha skrini ya ukaguzi wa waraka.
Teua ili kuonyesha ukaguzi wa ukurasa.
skrini ya uhakiki wa ukurasa
: Hupunguza au kuongeza.
: Huzungusha picha upande wa kulia kwa digrii 90.
: Husogeza skrini katika mwelekeo wa vishale.
: Husonga kwa ukurasa wa awali au unaofuata.
Ili kuficha ikoni za operesheni, donoa mahali popote kwenye skrini ya uhakiki isipokuwa kwa ikoni. Donoa tena ili kuonyesha ikoni.
Endelea Kuchapisha
Huchapisha waraka unaokagua kwanza.
Unaweza kuweka mipangilio kama vile ya Nakala kabla ya kuanza kuchapisha. Kumbuka kuwa baadhi ya vipengee vya kuweka vinahitaji bidhaa za hiari.
Futa
Hufuta waraka unaokagua kwanza.
Maelezo
Huonyesha maelezo ya waraka uliochaguliwa kama vile tarehe na muda uliohifadhiwa na jumla ya idadi ya kurasa.
Tuma/Hifadhi
Unaweza kutekeleza operesheni zifuatazo kwa waraka ulioteuliwa.
Tuma Faksi
Sambaza(Barua pepe)
Tuma mbele(Kabrasha la Mtandao)
Tuma mbele (Wingu)
Hifadhi kwenye Kumbukumbu
Kutoka kwenye vipengee Sambaza(Barua pepe), Tuma mbele(Kabrasha la Mtandao), na Hifadhi kwenye Kumbukumbu, unaweza kuteua PDF au TIFF katika Umbizo la Faili unapohifadhi au kusambaza nyaraka. Unapoteua PDF unaweza kuweka mipangilio ifuatayo kwenye Mipangiliuo ya PDF inavyohitajika.
Nenosiri la Kufungua Hati
Nenosiri la Vibali la Uchapishaji na Kuhariri
Wakati ujumbe Futa Ikikamilika unaonyeshwa, teua Washa ili kufuta faksi baada ya kukamilisha michakato kama vile Sambaza(Barua pepe) au Hifadhi kwenye Kumbukumbu.
Futa
Hufuta waraka ulioteuliwa.
Nyingine
Jina la Faili: Huweka jina la nyaraka iliyochaguliwa.
(Menyu ya Kasha)
Chapisha Zote
Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huchapisha faksi zote kwenye kikasha. Unaweza kuweka mipangilio ya uchapishaji. Tazama ufafanuzi katika Mipangilio ya Chapa kwenye ukurasa huu.
Hifadhi Zote kwenye Kifaa cha Kumbukumbu
Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huhifadhi faksi zote kwenye vifaa vya kumbukumbu ya nje kwenye kikasha.
Unaweza kuteua PDF au TIFF kwenye Umbizo la Faili unapohifadhi au kusambaza waraka. Unapoteua PDF unaweza kuweka mipangilio ifuatayo kwenye Mipangiliuo ya PDF inavyohitajika.
Nenosiri la Kufungua Hati
Nenosiri la Vibali la Uchapishaji na Kuhariri
Kuteua Washa kwenye Futa Ikikamilika hufuta nyaraka zote wakati kuhifahi kumekamilika.
Futa Zote Zilizosomwa
Hii huonyeshwa tu wakati kuna nyaraka kwenye kikasha. Hufuta nyaraka zote kwenye kisanduku.
Futa Zote Ambazo Hazijasomwa
Hii huonyeshwa tu wakati kuna nyaraka kwenye kikasha. Hufuta nyaraka zote ambazo hazijasomwa zilizo kwenye kikasha.
Futa Zote
Hii inaonyeshwa tu wakati kuna nyaraka za faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Hufuta faksi zote kwenye kikasha.
Chaguo wakati kumbukumbu imejaa: teua chaguo moja ili kuchapisha au kukataa faksi zinazoingia baada ya Kikasha pokezi kujaa.
Mipangilio ya Nenosiri la Kisanduku pokezi: Unaweza kuweka nenosiri au kulibadilisha.
Futa Faksi Zilizopokewa Kiotomatiki: Kuteua Washa kiotomatiki hufuta nyarak za faksi iliyopokewa kwenye kikasha pokezi baada ya muda fulani. Wakati Fuata Mipangilio ya Faksi imetueliwa, mipangilio ifuatayo inatumika.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Mipangilio ya Kawaida > Mipangilio ya Kisanduku ya Kufuta Hati
Vipengee vifuatavyo vinaonyeshwa unapoteua kikasha cha siri na kuteua Menyu ya Kasha > Mipangilio.
Jina: ingiza jina la kikasha cha siri.
Nywila ya Kufungua Kikasha: Unaweza kuweka nenosiri au kulibadilisha.
Futa Faksi Zilizopokewa Kiotomatiki: Kuteua Washa kiotomatiki hufuta nyarak za faksi iliyopokewa kwenye kikasha pokezi baada ya muda fulani.
Futa Kasha
Kipengele hiki kinaonyeshwa tu wakati unachagua kisaduku cha siki na uchague Menyu ya Kasha. Hufuta mipangilio ya sasa ya Visaduku vya Siri na hufuta hati zote zilizohifadhiwa.
Nakala
Weka idadi ya nakala za kuchapisha.
Teua Ukurasa
Teua kurasa unazotaka kuchapisha.
Mipangilio ya Chapa
Unaweza kuweka vipengee vifuatavyo.
Kumbuka kuwa baadhi ya vipengee vya kuweka vinahitaji bidhaa za hiari.
Pande 2
Pande 2:
Weka ikiwa utachapisha au kutochapisha hati za kurasa nyingi kwenye kisanduku cha pande zote mbili za karatasi.
Pambizo ya Kufunga:
Teua nafasi ya uunganishaji kwa uchapishaji wa pande 2.
Kumalizia
Kumalizia
Toa Karatasi
Bana kwa stepla
Toboa
Mkunjo Nusu
Mkunjo Mara Tatu
Kunja
Weka mipangilio ya vipengee vifuatavyo.
Mkunjo Nusu
Mkunjo Nusu
Hukuruhusu kufanya nakala zikunjwe nusu.
Kurasa kwa kila Kunja
Bainisha idadi ya kurasa za kukunja nusu.
Hali ya Kuchapisha
Teua ikiwa eneo la kuchapisha litakuwa ndani au nje ya karatasi inapokunjwa katikati.
Mkunjo Mara Tatu
Mkunjo Mara Tatu
Hukuruhusu kufanya nakala zikunjwe mara tatu.
Kurasa kwa kila Kunja
Bainisha idadi ya kurasa zilizokunjwa mara tatu.
Hali ya Kuchapisha
Teua ikiwa eneo la kuchapisha litakuwa ndani au nje ya karatasi inapokunjwa mara tatu.
Kufunga
Teua mwelekeo wa kuweka pamoja.
Trei ya Towe
Chagua trei moja ya towe kutoka kwa chaguo zilizoonyeshwa. Menyu huonyeshwa tu wakati kikamilishi cha stepla au trei ya ndani imesakinishwa.
Futa baada ya Kuchapisha
Hii ikiteuliwa, waraka ulioteuliwa unafutwa uchapishaji unapokamilika.