Kuweka Sauti

Weka mipangilio ya sauti unapotumia paneli dhibiti, kuchapisha, kutuma faksi na mengineyo.

Kumbuka:

Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Sauti

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Device Management > Sound

  4. Weka vipengee vifuatavyo inavyohitajika.

    • Normal Mode
      Weka sauti kichapishi kinapowekwa katika Normal Mode.
    • Quiet Mode
      Weka sauti kichapishi kinapowekwa katika Quiet Mode.
      Hii huwezeshwa wakati mojawapo ya vipengee vifuatavyo kimewezeshwa.
      • Paneli dhibiti ya kichapishi:
        Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Hali Tulivu
        Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Chapa > Hali Tulivu
      • Web Config:
        Kichupo cha Fax > Print Settings > Quiet Mode
  5. Bofya OK.