Unaweza kuweka huduma ya utambazaji wa mtandao ukitambaza kutoka kwa kompyuta ya mteja kwenye mtandao. Mpangilio wa chaguo-msingi umewezeshwa.
Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya
Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.
Teua kwenye orodha inayofuata.
Scan/Copy kichupo > Network Scan
Hakikisha kuwa Enable scanning ya Epson Scan 2 imeteuliwa.
Ikiwa imeteuliwa, kazi hii imekamilika. Funga Web Config.
Ikifutwa, iteue na uende kwenye hatua inayofuata.
Bofya Next.
Bofya OK.
Mtandao umeunganishwa tena, na kisha mipangilio ikawezeshwa.