Unaweza kulemaza kiolesura kinachotumika kuunganisha kifaa kwenye kichapishi. Weka mipangilio ya vizuizi ili kuzuia uchapishaji na utambazaji kwa njia tofauti na kupitia mtandao.
Udhibiti wa kituo tayarishi cha USB: hupunguza uwezekano wa data kufanyiwa utambazaji usioidhinishwa wa hati za siri.
Uunganishaji wa USB kwenye kompyuta: huzuia matumizi ya kifaa bila idhini kwa kuzuia uchapishaji au utambazaji bila kupitia kwenye mtandao.
Pia unaweza kuweka mipangilio ya vizuizi kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Memory Device: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Kifaa cha Kumbukumbu
M'nisho wa Ko'ta kupitia USB: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > M'nisho wa Ko'ta kupitia USB
Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya
Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.
Teua kwenye orodha inayofuata.
Kichupo cha Product Security > External Interface
Teua Disable kwenye vitendaji unavyotaka kuweka.
Teua Enable unapotaka kughairi udhibiti.
Bofya OK.
Hakikisha kwamba kituo kilicholemazwa hakiwezi kutumika.