> Katika Hali Hizi > Kuunganisha Moja kwa Moja kwenye Kichapishi (Wi-Fi Direct) > Kuunganisha kwenye iPhone, iPad au iPod touch kwa kutumia Wi-Fi Direct

Kuunganisha kwenye iPhone, iPad au iPod touch kwa kutumia Wi-Fi Direct

Mbinu hii hukuruhusu kuunganisha kichapishi moja kwa moja kwenye iPhone, iPad au iPod touch bila kipanga njia rahisi.

Unahitaji kusakinisha Wireless LAN Interface-P1 ya hiari ili utumie kipengele hiki.

Masharti yafuatayo yanahitajika ili kutumia kitendaji hiki. Iwapo mazingira yako hayalingani na masharti haya, unaweza kuunganisha kwa kuteua Vifaa Vingine vya OS. Tazama kiungo cha maelezo husiani hapa chini kwa ufafanuzi kuhusu kuunganisha.

  • iOS 11 au toleo la baadaye

  • Kutumia programu ya kamera wastani ili kutambaza msimbo wa QR

  • Epson Smart Panel Toleo la 4.00 au la baadaye

Chapisha kutoka katika kifaa chako maizi ukitumia Epson Smart Panel. Sakinisha Epson Smart Panel kwenye kifaa maizi mapema.

Kumbuka:

Unahitaji kuunda mipangilio hii kwa kichapishi na kifaa maizi unachotaka kuunganisha mara moja. Isipokuwa ulemaze Wi-Fi Direct au kurejesha mipangilio ya mtandao kwa chaguo-msingi yake, huhitaji kuunda mipangilio hii tena.

  1. Donoa kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Teua Wi-Fi Direct.

  3. Teua Anza Kusanidi.

  4. Teua iOS.

    Msimbo wa QR unaonyeshwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  5. Kwenye iPhone, iPad au iPod touch yako, washa programu ya Kamera wastani, na kisha utambaze msimbo wa QR unaoonyeshwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi kwenye modi ya PICHA.

    Tumia programu ya Kamera kwa toleo la iOS 11 au la baadaye. Huwezi kuunganisha kichapishi kwa kutumia programu ya Kamera kwa toleo la iOS 10 au la mapema. Pia, huwezi kuunganisha kwa kutumia programu ya kutambaza misimbo ya QR. Iwapo huwezi kuunganisha, teua Vifaa Vingine vya OS kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Tazama kiungo cha maelezo husiani hapa chini kwa ufafanuzi kuhusu kuunganisha.

  6. Donoa taarifa ya kuunganisha iliyoonyeshwa kwenye skrini ya iPhone, iPad, au iPod touch.

  7. Donoa Jiunge.

  8. Hakikisha kuwa ujumbe unaoonyesha kwamba muunganisho umeanzishwa unaonyeshwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, kisha uguse Sawa.

  9. Teua Imekamilika.

  10. Kwenye iPhone, iPad au iPod touch, anzisha Epson Smart Panel.

    Epson Smart Panel huongeza kiotomatiki vichapishi vilivyounganishwa kwenye kifaa chako maizi. Fuata maagizo ya kwenye skrini.

Kwa vifaa maizi ambavyo vimeunganishwa kwenye kichapishi mbeleni, teua jina la mtandao (SSID) kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa maizi ili kuviunganisha tena.