Kuleta Waasiliani kwa Kutumia Web Config

Iwapo una kichapishi kinachokuruhusu kucheleza waasiliani na kinapatana na kichapishi hiki, unaweza kusajili waasiliani rahisi kwa kuleta faili ya chelezo.

Kumbuka:

Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuhifadhi waasiliani wanaoendana na kichapishi hiki, tazama wa waraka uliotolewa na kichapishi kilicho na orodha ya waasiliani inayopatana na kichapishi hiki.

Fuata hatua zilizo hapa chini ili kuleta waasiliani kwenye kichapishi.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya mtandao (kamili/wa ziada) ambao unataka kusanidi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani au Ya Ziada) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Device Management > Export and Import Setting Value > Import

  4. Teua faili ya chelezo uliyoiunda kwenye File, ingiza nenosiri, na kisha ubofye Next.

  5. Teua kikasha teuzi cha Contacts, na kisha ubofye Next.