Kusanidi Cheti kwa ajili ya IEEE 802.1X

Sanidi Chrti cha Mteja kwa ajili ya IEEE802.1X. Unapoiweka, unaweza kutumia EAP-TLS na PEAP-TLS kama mbinu ya uidhinishaji wa IEEE 802.1X. Iwapo unataka kusanidi cheti cha mamlaka ya uidhinishaji, nenda kwenye CA Certificate.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya mtandao (kamili/wa ziada) ambao unataka kusanidi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani au Ya Ziada) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Network Security > IEEE802.1X > Client Certificate

  4. Ingiza cheti kwenye Client Certificate.

    Iwapo tayari umeleta cheti kilichochapishwa na Mamlaka ya Uidhinishaji, unaweza kunakili cheti na ukitumie kwenye IEEE802.1X. Ili kunakili, teua cheti kutoka Copy From, kisha ubofye Copy.