Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya mtandao (kamili/wa ziada) ambao unataka kusanidi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani au Ya Ziada) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya
Ingiza nenosiri kisha ubofye OK.
Teua kwenye orodha inayofuata.
Device Management kichupo > Control Panel
Kwenye Panel Lock, teua ON.
Bofya OK.
Angalia kwamba
imeonyeshwa kwenye skrini ya nyumbani kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.