Unaposajili mpokeaji kwenye orodha ya wasiliani, unaweza kuteua IP-FAX kama mpangilio wa laini.
Teua menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Kisimamia Waasiliani
Teua Ongeza/Hariri/Futa.
Fanya moja kati ya zifuatazo.
Teua Faksi kutoka kwa chaguo za aina zilizoonyeshwa.
Huwezi kubadilisha aina baada ya kukamilisha usajili. Iwapo unataka kubadilisha aina, futa ufikio na usajili tena.
Teua Nambari ya Faksi (Inahitajika).
Teua IP-FAX kwenye Ch. Mstari.
Ingiza ufikio.
Teua Sawa ili kutekeleza mipangilio.