> Maelezo ya Msimamizi > Kudhibiti Kichapishi > Kuweka Paneli Dhibiti

Kuweka Paneli Dhibiti

Usanidi wa paneli dhibiti ya kichapishi. Unaweza kusanidi kama ifuatavyo.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Device Management > Control Panel

  4. Weka vipengee vifuatavyo inavyohitajika.

    • Language
      Teua lugha iliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti.
    • Panel Lock
      Iwapo utateua ON, huwezi kuteua vipengee vinavyohitaji mamlaka ya msimamizi. Ili kuviteua, ingia kwenye kichapishi kama msimamizi.
    • Operation Timeout
      Ukiteua ON, unaenda kwenye skrini ya awali ikiwa hakuna shughuli kwa kipindi fulani cha muda.
      Unaweza kuweka kati ya sekunde 10 na dakika 240 kulingana na sekunde.
    • Theme Color
      Chagua rangi ya mandhari ya skrini ya LCD kwenye orodha.
    • Display during printing
      Chagua kipengee cha kuonyeshwa kwenye skrini ya LCD wakati wa kuchapisha.
    • Custom(Message)
      Wakati Custom(Message) inachaguliwa katika Display during printing, bainisha maandishi unayotaka kuonyesha. Unaweza kuingiza hadi vibambo 400.
    • Custom(Image)(Maximum 856x502px, 200KByte, PNG)
      Wakati Custom(Image) inachaguliwa katika Display during printing, sajili na ufute picha ambazo ungependa kuonyesha.
    Kumbuka:

    Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    • Language: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Lugha/Language

    • Operation Timeout: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Muda wa Shughuli Umeisha (Unaweza kubainisha Kuwasha au Kuzima).

    • Rangi ya Mandhari: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Rangi ya Mandhari

    • Display during printing: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Hariri Ukurasa wa Nyumbani

  5. Bofya OK.