Kutumia Document Capture Pro Server, sanidi Server Mode kutoka Web Config.
Unaweza pia kuweka Server Mode kutoka kwenye paneli dhibiti kwa kufikia menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Uchanganuzi > Programu ya Unasaji Waraka > Hali ya Matumizi
Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya
Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.
Teua kwenye orodha inayofuata.
Kichupo cha Scan/Copy > Document Capture Pro
Teua Server Mode kwa Mode.
Ingiza anwani ya seva iliyo na Document Capture Pro Server ambayo imesakinishwa ndani yake kwa ajili ya Server Address.
Ingiza vibambo kati ya 2 na 255 vya ama umbizo la IPv4, IPv6, jina la mpangishaji au FQDN. Kwa umbizo la FQDN, unaweza kutumia vibambo vya nambari na abjadi katika ASCII (0x20–0x7E) na “- ” isipokuwa mwanzoni na mwishoni mwa anwani.
Bofya OK.
Mtandao umeunganishwa tena, na kisha mipangilio ikawezeshwa.