Unaposajili mpokeaji kwenye orodha ya waasiliani, unaweza pia kuongeza mpangilio wa laini.
Teua menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Kisimamia Waasiliani
Teua Ongeza/Hariri/Futa.
Fanya moja kati ya zifuatazo.
Teua Faksi kutoka kwa chaguo za aina zilizoonyeshwa.
Huwezi kubadilisha aina baada ya kukamilisha usajili. Iwapo unataka kubadilisha aina, futa ufikio na usajili tena.
Teua Nambari ya Faksi (Inahitajika).
Chagua laini kwenye Ch. Mstari, kisha uteue Funga.
Ingiza ufikio.
Teua Sawa ili kutekeleza mipangilio.