> Utangulizi wa Vipengele Mahiri > Epson Print Admin Serverless > Muhtasari wa Epson Print Admin Serverless

Muhtasari wa Epson Print Admin Serverless

Epson Print Admin Serverless hutoa mazingira salama na mwafaka ya kutumia vichapishaji kwenye mitandao kama vile ya ofisi au shule.

Masuluhisho yafuatayo yanapatianwa.

  • Usalama Ulioboreshwa

    Watumiaji walioidhinishwa pekee ndio wanaweza kutumia kichapishi.

    Unaweza kuzuia hati za siri kuchukuliwa na wafanyakazi ambao hawajaidhinishwa, kuchanganya hati na za watumiaji wengine, na kadhalika kwa vile zimechapishwa kutoka kwa kichapishi kilichoidhinishwa.

  • Akiba ya Gharama

    Unaweza kuzuia uchapishaji usio wa lazima kwani kazi za uchapishaji huchaguliwa moja kwa moja kutoka kwenye orodha ya kazi.

  • Ufanisi wa Biashara

    Bila kufanya shughuli zozote tatanishi, unaweza kutuma data iliyochanganuliwa kwa anwani yako ya baruapepe au kuhifadhi kwenye folda lengwa lililosajiliwa.

  • Kipengele cha Udhibiti kwa Urahisi

    Unaweza kuweka maelezo kwa watumiaji wengi kwa wakati mmoja, au kuweka vipengel vinavyoweza kutumika kwa kila mtumiaji. Ukiwa na Epson Device Admin, unaweza kudhibiti vichapishaji vingi kwa pamoja, kulandanisha na seva ya LDAP, na kuunda ripoti za historia ya matumizi kiotomatiki.