Ili kutumia usimbaji fiche wa barua pepe, unahitaji kuleta cheti cha usimbaji fiche kwenye kila ufikio uliosajiliwa kwenye orodha ya waasiliani.
Sehemu hii inaeleza utaratibu wa kuleta cheti cha usimbaji fiche kwenye kila ufikio wa barua pepe uliosajiliwa kwenye orodha ya waasiliani.
Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya
Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.
Teua kwenye orodha inayofuata.
Scan/Copy au kichupo cha Fax > Contacts
Teua namabri ya ufkio ambapo unataka kuleta cheti chako cha usimabji fiche, kisha ubofye Edit.
Leta cheti cha usimbaji fiche kwenye ufikio kwa Encryption Certificate au Change encryption certificate.
Bofya Apply.
Wakati cheti cha usimbaji fiche kimeletwa, aikoni ya ufungua huonyeshwa kwenye orodha ya waasiliani.
Unaweza kuangalia maelezo ya cheti kuhusu Encryption certificate status kwa kuteua namabri ya ufikio ambapo umeleta cheti chako cha usimbaji fiche na kubofya Edit.