Kusambaza Mipangilio ya Kupokea Faksi kwa Masharti Yaliyobainishwa

Unaweza kuweka mipangilio ya usambazaji ili kupokea faksi kutoka kwa mtumaji aliyebainishwa au muda uliobainishwa.

Wakati hali nyingi (Masharti ya Hifadhi/Sambaza) zimewekwa, zimerejelewa katika mpangilio wa vipengee, na Masharti ya Hifadhi/Sambaza inayolingana kwanza inatekelezwa.

Unaweza kuweka mipangilio ya usambazaji hadi eneo, anwani ya barua pepe, folda ya pamoja, akaunti ya wingu au mashine nyingine ya faksi kutoka kwa mtumaji aliyebainishwa au muda uliobainishwa.

Kumbuka:
  • Iwapo unataka kufanya mipangilio ya kusambaza faksi zilizopokewa, kwanza ongeza anwani inayosambazwa kwenye orodha ya anwani au orodha ya anwani ya wingu. Tazama jedwali linalofuata ili kupata orodha ya kusajili.

    Aina ya Ufikio

    Waasiliani

    Wingu Orodha ya Mafikio

    anwani ya barua pepe

    folda ya pamoja

    akaunti ya wingu

    mashine nyingine ya faksi

Kuweka Mipangilio ya Usambazaji ili Kupokea Faksi kwa Masharti Yaliyobainishwa

Kumbuka:
  • Kando na kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, unaweza kutumia Web Config kuweka mipangilio ya usambazaji ili kupokea faksi. Teua kichupo cha Fax > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, teua nambari ya kisanduku cha siri na kisha uteue Edit na uweke mipangilio ya eneo la kusambazia.

  • Unaweza kuchapisha na/au kuhifadhi faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja. Weka mipangilio kwenye skrini ya Edit iliyotajwa hapa juu.

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti yakichapishi, kisha uteue Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi.

  2. Teua Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, kisha gusa kisanduku ambacho hakijasajiliwa chini ya Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

    Kumbuka:

    Ikiwa ungependa kubadilisha mipangilio ya kisanduku kilichosajiliwa, gusa na ubadilishe mipangilio.

  3. Teua kikasha cha Jina (Inahitajika) na uingize jina unalotaka kusajili.

  4. Teua kikasha cha Hali ili kuunda mpangilio wa masharti.

    • Ulinganisho wa Kitambulisho cha Faksi cha Mtumaji: iwapo kitambulisho cha mtumaji kinalingana na masharti uliyoteua kwenye kipengee hiki, printa husambaza faksi iliyopokewa.
      Teua KITAMBULISHO, na kisha uweke kitambulisho cha mtumaji, kama vile nambari yao ya faksi.
      Faksi ya IP ikiwezeshwa, unaweza pia kuteua SIP URI au nambari ya faksi kama kitambulisho kutoka kwenye orodha ya wasiliani.
    • Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO): iwapo anwani ndogo (SUB) inawiana vilivyo, printa husambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO) na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Anwani ndogo(NDOGO).
    • Ulinganishaji kamili wa nywila: iwapo nenosiri (SID) limewianishwa vilivyo, printa husambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Ulinganishaji kamili wa nywila na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Nywila(SID).
    • Mlinganisho wa Mstari Uliopokewa: Inapatikana wakati bodi ya ziada ya faksi inasakinishwa au Faksi ya IP kuwezeshwa upya. Iwapo kituo cha laini kinalingana, kichapishi husambaza faksi zilizopokewa.
    • Wakati wa Kupokea: printa husambaza faksi zilizopokewa wakati wa kipindi maalum cha muda.
      Wezesha mpangilio wa Wakati wa Kupokea na kisha uweke muda katika Muda wa Kuanza na Muda wa Mwisho.
  5. Teua Hifadhi/Mfikio wa Kusambaza (Inahitajika), na kisha uweke mipangilio ya eneo la kusambazia.

    Teua Sambaza.

    Donoa Sambaza ili kuweka hii kwa Washa.

    Teua Ongeza Ingizo, kisha uteue maeneo ya kusambazia kutoka kwenye orodha yako ya wasiliani au orodha ya ufikio wa wingu. Unaweza kubainisha anwani ya usambazaji.

    Kubadilisha orodha, gusa Wingu Orodha ya Mafikio au Waasiliani.

    Ukimaliza kuchagua anwani za usambazaji, gusa Funga.

    Hakikisha kwamba anwani ya usambazaji uliyochagua ni sahihi, na kisha uchague Funga.

    Katika Chaguo Wakati Us'zaji Um'dikana, chagua kama unataka kuchapisha hati zilizopokewa au kuzihifadhi katika Kisanduku pokezi ya kichapishi wakati usambazaji unakosa kufaulu.

    Teua Sawa.

    Muhimu:

    Wakati Kisanduku pokezi au kisanduku cha siri kimejaa, upokeaji wa faksi unalemazwa. Unastahili kufuta hati kwenye kisanduku pokezi punde tu zinapoangaliwa. Idadi ya nyaraka ambazo zilishindwa kusambaza imeonyeshwa kwenye katika skrini ya nyumbani, kwa kuongezea kwenye kazi zingine zisizochakatwa.

    Kumbuka:

    Ili kuchapisha faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja, donoa Chapisha ili uweke hii iwe Washa.

  6. Teua Sawa ili ukamilishe Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza Mfikio.

    Kumbuka:

    Unaweza kuweka kichapishi kitume barua pepe kwa watu unaotaka kuwaarifu kuhusu matokeo ya usambazaji wa faksi wakati mchakato wa usambazaji ukikamilika. Ilivyo muhimu, teua Taarifa za Barua pepe, weka michakato na kisha uteue eneo unapotaka kutuma arifa kutoka kwenye orodha ya waasiliani.

  7. Teua Sawa hadi urejee kwenye skrini ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza ili kukamilisha Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

  8. Teua kisanduku kilichosajiliwa ambacho ulifanya mpangilio wa masharti, na kisha uteue Wezesha.

Hii hukamilisha uwekaji mipangilio ya uhifadhi wa masharti ya kupokea faksi. Unaweza kuweka Mipangilio ya Kawaida ilivyo muhimu. Kwa maelezo, angalia ufafanuzi wa Mipangilio ya Kawaida katika menyu ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza.

Kumbuka:
  • Hii hukamilisha uwekaji mipangilio ya usambazaji wa masharti ya kupokea faksi. Unaweza kuweka Mipangilio ya Kawaida ilivyo muhimu. Kwa maelezo, angalia ufafanuzi wa Mipangilio ya Kawaida katika menyu ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza.

Kukagua Ufikio wa Usambazaji

Ikiwa umechagua kabrasha la kushiriki kwenye mtandao, anwani ya barua pepe, au akaunti ya wingu kama mafikio wa usambazaji, tunapendekeza kwamba ujaribu kama unaweza kutuma picha hadi kwa ufikio.

Teua Changanua > Barua pepe, Changanua > Folda/FTP ya Mtandao kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, teua mafikio, na kisha anzisha utambazaji.

Ikiwa umeteua akaunti ya wingu, unaweza kufanya jaribio kwa kutuma picha ambayo imehifadhiwa katika kisanduku cha faksi kwenye ufikio huo. Teua Kasha la Faksi fkutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, na uteue kikasha ambacho picha imehifadhiwa. Teua Tuma/Hifadhi > Tuma mbele (Wingu), teua ufikio, na kisha uanze kusambaza.