Kusajili VolP Gateway

Sajili VolP gateway unayotaka kutumia ili kutuma na kupokea faksi za IP.

  1. Fikia Web Config, na kisha uteue kichupo cha Fax > IP-FAX Settings > VoIP Gateway Settings.

  2. Bofya Registered VoIP Gateway > Edit.

    Skrini inayoonyesha orodha za VoIP gatewau zilizosajiliwa inaonyeshwa.

  3. Teua idadi unayotaka kusajili au kuhariri, na kisha ubofye Edit.

  4. Teua kila kipengee.

    • Name
      Ingiza jina la VoIP gateway ukitumia hadi vibambo 30 vinavyoweza kuonyeshwa katika UTF-16. Hata hivyo, vibambo vya kudhibiti (0x00 hadi 0x1F na 0x7F) haviwezi kutumika.
    • IP Address
      Ingiza jina la mwenyeji au anwani ya IP ya VoIP gateway. Unaweza kuingiza vibambo 0 hadi 127 ambavyo vinaweza kuonyeshwa katika ASCII (0x20 hadi 0x7E). Hata hivyo, huwezi kutumia nafasi au vibambo vifuatavyo: "<>\^`{¦}
    • Port Number
      Ingiza nambari ya kituo ya VoIP gateway ukitumia nambari za baiti moja kati ya safu 1 hadi 65535.
  5. Bofya OK.

    Mipangilio inaakisiwa kwenye printa.