Tahadhari za Kushughulikia Kibweta cha Wino

Soma maelekezo yafuatayo kabla ya kubadilisha vibweta vya wino.

Kuhifadhi tahadhari kwa wino
  • Weka katriji za wino mbali na mwale wa jua wa moja kwa moja.

  • Usihifadhi katriji za wino katika halijoto za juu au zinazoganda.

  • Kwa matokeo bora kabisa, Epson inapendekeza utumie katriji ya wino kabla ya tarehe ya bora kabla iliyochapishwa kwenye kifurushi, au ndani ya mwaka moja wa usakinishaji, wowote ambao ni rahisi zaidi.

  • Baada ya kuleta katriji ya wino ndani kutoka eneo, iwache ipate joto kwa halijoto ya chumba kwa angalau saa tatu kabla ya kuitumia.

Tahadhari za shughuli ya kubadilisha katriji za wino
  • Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye picha. Kufanya hivyo kunaweza kuzuia utendaji na uchapishaji wa kawaida.

  • Usifungue pakiti ya katrji ya wino hadi uwe tayari kuweka ndani ya printa. Katriji hupakiwa bila hewa ili kudumisha utumikaji wake. Ukiiwacha katriji ikiwa haijapakiwa kwa muda mrefu kabla ya kuitimia, uchapishaji wa kawaida huenda usiwezekane.

  • Usiiangushe au kuigongesha katika vitu vugumu; la sivyo wino unaweza kuvuja.

  • Funga katriji zote za wino; la zivyo hutaweza kuchapisha.

  • Usizime printa wakati wa kunyonya wino. Ikiwa unyonyaji wa wino haujakamilika, huwezi kuchapisha.

  • Usiwache printa wakati katriji za wino zimeondolewa; la sivyo, wino uliobakia katika nozeli za kichwa cha kuchapisha utakauka na hutaweza kuchapisha.

  • Ikiwa unahitaji kuondoa katriji ya wino kwa muda, hakikisha umelinda eneo la kutoa wino kutokana na uchafu na vumbi. Hifadhi kibweta cha wino katika mazingira sawa na kichapishi, lango la kutoa wino likiwa linaangalia chini au kando. Kwa sababu lango la kutoa wino lina vali iliyoundwa kuzuia utoaji zaidi wa wino, hakuna haja ya kutumia vifuniko au plagi zako mwenyewe.

  • Katriji za wino zilizoondolewa huenda zikawa na wino kando ya lango la kutoa wino, kwa hivyo kuwa mwangalifu usipake wino wowote kwenye eneo lililo kando wakati wa kuondoa katriji.

  • Printa hii hutumia katriji zilizo na chipu ya kijani inayofuatilia maelezo kama vile kiwango cha wino kinachobakia kwa kila katriji. Hii inamaanisha kwamba hata kama katriji imeondolewa kutoka kwa printa kabla ya kumalizika, bado unaweza kutumia katriji hiyo baada ya kuiingiza upya katika printa.

  • Ili kuhakikisha unapata uchapishaji wa ubora wa juu na kusaidia kulinda kicha chako cha uchapishaji, akiba tofauti ya usalama ya wino hubakia katika katriji wakati printa yako inakuonyesha unafaa kubadilishwa katriji. Viwango vilivyoandikwa havijumuishi akiba hii.

  • Sifa na sura ya katriji ya wino zinaweza kubadilishwa bila notisi ili kuoboresha.

  • Usifungue au kubadilisha modeli ya katriji ya wino, la sivyo huenda usiweze kuchapisha kwa kawaida.

  • Huwezi kutumia katriji zilizokuja na printa kufanya mabadilisho.

  • Usiondoe au kusakinisha tena kibweta cha wino isipokuwa inapohitajika. Wino unaweza kuenea kwenye eneo lililo karibu ikiwa unaondolewa na kusakinishwa upya kwa marudio.

  • Hata iwapo baadhi ya vibweta vya wino vimebonyeka kutokana na mchakato wa kuvuta hewa, ubora na kiwango cha wino zimeahidiwa, na vinaweza kutumika kwa usalama. Usifungue pakiti ya kibweta cha wino hadi uwe tayari kubadilisha kibweta cha zamani.

Matumizi ya wino
  • Ili kudumisha utendaji mzuri wa kichwa cha kuchapisha, kiasi fulani cha wino hutumiwa kutoka kwa katriji zote wakati wa operesheni za matengenezo kama vile usafishaji wa kichwa cha kuchapisha. Pia wino unaweza kutumika unapowasha kichapishi.

  • Wakati unachapisha rangi moja au kijivujivu, wino wa rangu badala ya wino mweusi unaweza kutumiwa kulingana na aina ya karatasi au mipangilio ya ubora wa uchapishaji. Hii ni kwa sababu mchanganyiko wa wino wa rangu unatumiwa kutengeneza rangi nyeusi.

  • Viwango viliandikwa vinaweza kuwa tofauti kulingana na picha unazochapisha, aina ya karatasi unayotumia, marudio ya uchapishaji na hali ya mazingisa kama vile halijoto.

  • Wino katika katriji za wino zilizokuja na printa yako zimetumwa kwa kiasi fulani wakati wa usanidi wa mwanzo. Ili uchapishe nakala za hali ya juu, kichwa cha kuchapisha kilicho katika printa yako kitajazwa wino. Mchakato huu wa mara moja hutumia kiasi cha wino na basi katriji hizi zinaweza kuchapisha kurasa chache kulingana na katriji za wino zitakazofuata.