> Maelezo ya Msimamizi > Kudhibiti Kichapishi > Kusanidi Taarifa za Baruapepe Matukio Yakitokea

Kusanidi Taarifa za Baruapepe Matukio Yakitokea

Unaweza kusanidi taarifa za barua pepe ili barua pepe itumwe kwa anwani zilizotajwa matukio kama vile kusimama kwa uchapishaji au hitilafu za kichapishi zikitokea. Unaweza kusajili hadi ufikio tano na uweke mipangilio ya taarifa kwa kila ufikio.

Ili kutumia utendaji huu, unahitaji kusanidi seva ya barua pepe kabla ya kuweka mipangilio ya taarifa. Sanidi seva ya barua pepe kwenye mtandao (wa kawaida au wa ziada) ambapo ungependa kutuma barua pepe.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Device Management > Email Notification

  4. Weka mada ya taarifa ya barua pepe.

    Teua maudhui yanayoonyeshwa kwenye mada kutoka katika menyu mbili za kuvuta chini.

    • Maudhui yaliyoteuliwa yanaonyeshwa karibu na Subject.
    • Maudhui sawa hayawezi kuwekwa kwenye kushoto na kulia.
    • Idadi ya vibambo kwenye Location inapozidi biti 32, vibambo vinavyozidi biti 32 hufungiwa nje.
  5. Ingiza anwani ya barua pepe ya kutuma barua ya taarifa.

    Tumia A–Z a–z 0–9 ! # $ % & ' * + - . / = ? ^ _ { | } ~ @, na uingize vibambo kati ya vibambo 1 na 255.

    Kadi ya kiolesura cha mtandao wa ziada ikisakinishwa, teua Network Destination ili kubainisha mtandao ambamo tukio hilo lilitokea.

  6. Teua lugha kwa ajili ya taarifa za barua pepe.

  7. Teua kisanduku cha kuteua kwenye tukio unalotaka kupokea taarifa kulihusu.

    Idadi ya Notification Settings kinaunganishwa kwenye idadi ya Email Address Settings.

    Iwapo unataka taarifa itumwe kwenye anwani ya barua pepe ya nambari 1 katika Email Address Settings wakati kichapishi hakina karatasi, teua safu ya kisanduku cha uteuzi cha 1 katika mstari wa Paper out.

  8. Bofya OK.

    Thibitisha kwamba taarifa ya barua pepe itatumwa kwa kusababisha tukio.

    Mfano: chapisha kwa kubainisha Chanzo cha K'tasi ambapo karatasi haijawekwa.