Kuna njia mbili unazoweza kutuma picha zilizochanganuliwa kwa anwani maalum ya barua pepe: kwa kusanidi seva ya barua pepe au kwa kutumia huduma ya wingu ya Epson Connect.
Yafuatayo yanafafanua jinsi ya kusanidi seva ya barua pepe ili kutuma picha zilizochanganuliwa kwa barua pepe.
|
Operesheni Muhimu |
Eneo la Operesheni |
Fafanuzi |
|---|---|---|
|
1. Unganisha printa kwenye mtandao (Hii sio muhimu iwapo uliunganishwa kwenye mtandao wakati wa usanidi) |
Printa na kompyuta |
Unganisha printa kwenye mtandao. |
|
2. Sajili maelezo ya seva yako ya barua pepe kwenye printa |
Kompyuta (Web Config) aupaneli dhibiti ya printa |
Kipengele cha Changanua kwa Barua pepe kinakuruhusu kutuma picha zilizochanganuliwa kupitia seva ya barua pepe. Sajili maelezo ya seva ya barua pepe kwenye printa. |
|
3. Kukagua muunganisho wa seva ya barua pepe |
Kompyuta (Web Config) aupaneli dhibiti ya printa |
Jaribu muunganisho wa seva ya barua pepe. |
|
4. Sajili anwani ya barua pepe ya mpokeaji kwenye Contacts |
Kompyuta (Web Config) aupaneli dhibiti ya printa |
Sajili anwani ya barua pepe ya mpokeaji kwenye Contacts wa kichapishi. Hili hukuruhusu kuteua mpokeaji kutoka Contacts bila kuhitajika kuweka anwani yake ya barua pepe unapoachanganua. |
|
5. Changanua kutoka kwa paneli dhibiti |
Paneli dhibiti ya kichapishi |
Tekeleza uchanganuzi kutoka kwenye paneli dhibiti. |