Kuweka Makosa

Weka uonyeshaji wa hitilafu kwa ajili ya kifaa.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN/Wi-Fi ya Waya

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Print > Error Settings

  4. Teua kila kipengee.

    • Paper Size Notice
      Weka iwapo utaonyesha kosa kwenye paneli dhibiti wakati ukubwa wa karatasi wa chanzo kilichobanishwa cha karatasi ni tofauti na ukubwa wa karatasi wa data iliyochapishwa.
    • Paper Type Notice
      Weka iwapo utaonyesha kosa kwenye paneli dhibiti wakati aina ya karatasi wa chanzo kilichobanishwa cha karatasi ni tofauti na aina ya karatasi ya data iliyochapishwa.
    • Auto Error Solver
      Weka iwapo utakatisha kosa kiotomatiki iwapo hakuna matumizi kwenye paneli dhibiti kwa sekunde 5 baada ya kuonyesha kosa.
  5. Angalia mipangilio, na kisha ubofye OK.