Fonti za Code128 hutumia seti ya msimbo ya A, B, na C. Wakati seti ya msimbo wa laini ya vibambo imebadilishwa katikati ya laini, msimbo wa kubadilisha inawekwa kiotomatiki.
Urefu wa msimbo wa mwambaaa unarekebishwa kiotomatiki hadi 15% au zaidi ya jumla ya urefu wake, kulingana na kiwango cha Code128. Kwa sababu hii, ni muhimu kuweka angalau nafasi moja katika ya msimbo wa mwambaa na matini yaliyo karibu ili kuzuia kupita nafasi zilizoachwa.
Baadhi ya programu hufuta kiotomatiki nafasi zilizo mwishoni wa mistari au kubadilisha nafasi nyingi kwenye vichupo. Misimbo ya mwambaa iliyo na nafasi huenda isichapishwe ipasavyo kutoka kwenye programu ambazo hufuta nafasi kiotomatiki kutoka mwishoni mwa mistari au kubadilisha nafasi nyingi kuwa vichupo.
Unapochapisha misimbo mbili au zaidi ya mwambaa kwenye mstari mmoja, tenganisha misimbo ya mwambaa kwa kutumia kichupo au uteue tofauti na Fonti ya Msimbo wa Mwambaa na uweke nafasi. Iwapo nafasi imeingizwa huku fonti ya Code128 imechaguliwa, msimbo wa mwambaa hautakuwa sahihi.
|
Aina ya kibambo |
Vibambo vyote vya ASCII (jumla ya 95) |
|
Idadi ya vibambo |
Haina kikomo |
|
Ukubwa wa fonti |
26 pt hadi 96 pt. Ukubwa unaopendekezwa ni 26 pt, 52 pt na 78 pt. |
Misimbo ifuatayo inaingizwa kiotomatiki na haihitaji kuwekwa kwa mkono:
Eneo tuli la Kushoto/Kulia
Kibambo cha Kuanza/Kukoma
Kuangalia herufi
Kubadilisha kibambo cha seti ya msimbo
Kuchapisha sampuli
|
EPSON Code128 |
![]() |