Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili
Kijitabu
Kijitabu
Bainisha mipangilio hii unapotaka kuunda kijitabu kutoka kwenye nakala zako.
Kijitabu
Hukuruhusu kuunda kijitabu kutoka kwenye nakala zako.
Kufunga
Teua nafasi ya uunganishaji wa kijitabu.
Pambizo ya Ufungaji
Teua ukingo wa kuunganisha. Unaweza kuweka 0 hadi 50 mm kuwa ukingo wa uunganishaji kwa uongenezaji wa 1 mm.
Jalada
Hukuruhusu kuongeza majalada kwenye kijitabu.
Saizi ya Hati
Chagua ukubwa wa nakala yako ya kwanza.
Mipangilio ya K'si
Teua chanzo cha karatasi unachotaka kutumia ili kuchapisha.
Pande 2
Teua muundo wa pande 2.
Taraza
Bainisha mipangilio hii unapotaka kufanya nakala kutarazwa mshono.
Menyu hii inaonyeshwa tu wakati kitendaji cha utarazaji mshono kimewezeshwa.
Taraza
Hukuruhusu kutaraza mshono wa nakala.
Kurasa kwa kila Kibanio
Bainisha idadi ya kurasa za kutaraza mshono.
Gawanya
Hukuruhusu kuchapisha kando.
Jalada
Hukuruhusu kuongeza majalada kwenye nakala.
Mipangilio ya K'si
Chagua chanzo cha karatasi ulichoweka karatasi kwa ajili ya majalada.
Mkunjo Nusu
Bainisha mipangilio hii unapotaka kufanya nakala zikunjwe nusu.
Menyu hii inaonyeshwa tu wakati kitendaji cha ukunjaji nusu kimewezeshwa.
Mkunjo Nusu
Hukuruhusu kufanya nakala zikunjwe nusu.
Kurasa kwa kila Kunja
Bainisha idadi ya kurasa za kukunja nusu.
Gawanya
Hukuruhusu kuchapisha kando.
Jalada
Hukuruhusu kuongeza majalada kwenye nakala.
Mipangilio ya K'si
Chagua chanzo cha karatasi ulichoweka karatasi kwa ajili ya majalada.
Hali ya Kuchapisha
Teua iwapo utachapisha nje au ndani ya karatasi nusu lililokunjwa.
Kunja
Mkunjo Nusu
Bainisha mipangilio hii unapotaka kufanya nakala zikunjwe nusu.
Menyu hii inaonyeshwa tu wakati kitendaji cha ukunjaji nusu kimewezeshwa.
Mkunjo Nusu
Hukuruhusu kufanya nakala zikunjwe nusu.
Kurasa kwa kila Kunja
Bainisha idadi ya kurasa za kukunja nusu.
Gawanya
Hukuruhusu kugawanya nakala zinapoondolewa.
Jalada
Hukuruhusu kuongeza majalada kwenye nakala.
Mipangilio ya K'si
Chagua chanzo cha karatasi ulichoweka karatasi kwa ajili ya majalada.
Hali ya Kuchapisha
Teua iwapo utachapisha nje au ndani ya karatasi nusu lililokunjwa.
Mkunjo Mara Tatu
Bainisha mipangilio hii unapotaka kufanya nakala zikunjwe mara tatu.
Menyu hii huonyeshwa tu wakati kipengele cha kukunja mara tatu kimewezeshwa.
Mkunjo Mara Tatu
Hukuruhusu kufanya nakala zikunjwe mara tatu.
Kurasa kwa kila Kunja
Bainisha idadi ya kurasa zilizokunjwa mara tatu.
Hali ya Kuchapisha
Teua iwapo utachapisha nje au ndani ya karatasi lililokunjwa mara tatu.
Fungua mwelekeo
Teua mwelekeo ulio wazi.
Jalada la Ka. Kuingizwa
Jalada
Bainisha haya unapotaka kuongeza jalada kwenye nakala zako.
Jalada la Mbele
Hukuruhusu kuongeza majalada ya mbele kwenye nakala. Iwapo umepakia karatasi kwa ajili ya jalada, teua chanzo cha karatasi kwenye Mipangilio ya K'si. Iwapo hutaki kuchapisha kwenye jalada la mbele, teua Usichapishe katika Hali ya Kuchapisha.
Jalada la Nyuma
Hukuruhusu kuongeza majalada ya nyuma kwenye nakala. Iwapo umepakia karatasi kwa ajili ya jalada, teua chanzo cha karatasi kwenye Mipangilio ya K'si. Iwapo hutaki kuchapisha kwenye jalada la nyuma, teua Usichapishe katika Hali ya Kuchapisha.
Karatasi ya Kuingizwa
Bainisha mipangilio hii unapotaka kuingiza laha za kuzuia uchafu kwenye nakala zako.
Mwisho wa Kazi
Hukuruhusu kuingiza laha za kuzuia uchafu kwa kila kazi ya kunakili. Iwapo umepakia karatasi kwa ajili ya laha za kuzuia uchafu, teua chanzo cha karatasi kwenye Mipangilio ya K'si.
Mwisho wa Seti
Hukuruhusu kuingiza laha za kuzuia uchafu kwa kila kikundi. Iwapo umepakia karatasi kwa ajili ya laha za kuzuia uchafu, teua chanzo cha karatasi kwenye Mipangilio ya K'si. Unaweza pia kubanisha vipindi vya kuingiza laha za kuzuia uchafu kwenye Kurasa kwa kila Seti.
Mwisho wa Ukurasa au Sura
Hukuruhusu kuweka mipangilio ya kuingiza laha za kuzuia uchafu za sura kwenye kurasa unazotaka kuziingiza. Thamani za mpangilio zinahifadhiwa na kuonyeshwa kwenye orodha. Unaweza kukagua maelezo ya mipangilio kwa kuteua mpangilio kutoka kwenye orodha. Unaweza pia kuhariri au kufuta mpangilio.
Saizi ya Hati
Chagua ukubwa wa nakala yako ya kwanza. Unapoteua Tambua Otomatiki, ukubwa wa nakala yako asili inagunduliwa kiotomatiki. Unaponakili nakala asili zisizo za ukubwa wa kawaida, teua Iliyofasiliwa na Mtumiaji, kisha ubainishe ukubwa asili.
Na. Asili zina Mch'o
Unaweza kuweka mchanganyiko ufuatao wa ukubwa kwenye ADF kwa wakati mmoja. A3 na A4; B4 na B5. Unapotumia michanganyiko hii, nakala asili zinanakiliwa kwa ukubwa halisi wa nakala asili. Weka nakala zako asili kwa kupanga upana wa nakala asili kama ilivyoonyeshwa hapa chini.
Mwelekeo (Asili)
Teua mwelekeo wa nakala yako asili.
Kitabu →Kurasa2
Hunakili kurasa zenye pande mbili za kijitabu kwenye karatasi ya kando ya karatasi.
Teua ukurasa wa kijitabu wa kutambaza.
Endelea Kutambaza
Unaweza kuweka idadi kubwa ya nakala asili kwenye ADF katika bechi, na kuzitambaza kama kazi moja ya utambazaji.
Ubora wa Taswira
Rekebisha mipangilio ya taswira.
Ulinganuzi
Rekebisha tofauti kati ya mwangaza na sehemu za giza.
Kulowesha
Rekebisha udhahiri wa rangi.
Uwiano Mwekundu, Uwiano wa Kijani, Uwiano wa Bluu
Rekebisha wiani wa kila rangi.
Ukali
Rekebisha ufupisho wa taswira.
Udhibiti wa Rangi
Rekebisha toni ya rangi ya ngozi. Donoa + ili kuifanya baridi (kuongeza kijani) na udonoe - ili kuifanya joto (ongeza nyekundu).
Ondoa Mand'yuma
Teua ukolevu wa mandharinyuma. Donoa + ili kuongeza mwangaza (weupe) kwenye mandharinyuma na udonoe - ili kuikoleza (kuongeza weusi).
Iwapo utateua Otomatiki, rangi za mandharinyuma za nakala asili zimetambuliwa, na zinaondolewa au kufifishwa kiotomatiki. Haitekelezwi sahihi iwapo rangi ya mandharinyuma ni kolevu zaidi au haijatambulika.
Pambizo ya Kufunga
Fanya mipangilio kama vile nafasi ya uunganishaji, upana wa uunganishaji, na mwelekeo wa asili. Kutokana na sifa za kichapishi hiki, huwezi kunakili ndani ya mm 3 kutoka kwenye ukingo wa karatasi. Kwa hivyo, hata ikiwa pambizo ya uunganishaji imewekwa kuwa mm 3 au chini, kwa kweli kutakuwa na pambizo ya mm 3.
Unaweza pia kuteua jinsi ya kuunda pambizo la uunganishaji kwenye menyu zifuatazo.
Upa. wa Uf'ji
Hugeuza na kunakili picha kulingana na upana wa uunganishaji. Iwapo picha iliyo kwenye upande mkabala na pambizo la uunganishaji huendelea zaidi ya ukingo wa karatasi, data hiyo haichapishwi.
Pu. ili Itoshee Kar'i
Inanakili picha iliyotambazwa kwa ukubwa mdogo kwenye upana wa uunganishaji ili kutoshea ndani ya ukubwa wa karatasi. Iwapo thamani ya Punguza/Pangua ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi, huenda data ikachapishwa zaidi ya kingo za karatasi.
Futa Taswira Kwenye Pambizo
Inafuta picha ambapo pambizo la uunganishaji unaundwa ili kulinda upana wa pambizo la uunganishaji.
Pu. ili Itoshee Kar'i
Hunakili picha zilizotambazwa kwa ukubwa mdogo kuliko thamani ya Punguza/Ongeza ili kutoshea ndani ya ukubwa wa karatasi. Iwapo thamani ya Punguza/Ongeza ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi, huenda data ikachapishwa zaidi ya kingo za karatasi.
Ondoa Kivuli
Huondoa vivuli kwenye nakala asili inayoonekana kwenye nakala.
Fremu
Huondoa vivuli vinavyoonekana kwenye nakala unaponakili karatasi nene.
Katikati
Huondoa vivuli vinavyoonekana kwenye kituo cha nakala unaponakili kijitabu.
Ondoa Mash. Panchi
Huondoa mashino ya kufunga wakati wa kunakili.
Nakala ya Kadi ya ID
Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi.
Nakala ya Uthibitisho
Unapotengeneza nakala anuwai, unaweza kuanza kwa nakala moja ili kuangalia matokeo, na kisha kunakili mengine.
Trei ya Towe
Teua trei ya towe ya Kunakili. Menyu hii huonyeshwa wakati kihitimishi cha stepla kimesakinishwa.
Mhuri
Mhuri
Teua Washa ili kuchapisha mihuri kwenye nakala zako.
Aina
Chagua aina ya mhuri.
Nafasi ya Stempu
Chagua mkao wa mhuri.
Chapisha Ukurasa
Chagua ukurasa unaotaka kuchapisha mhuri.
Ukubwa
Chagua ukubwa wa mhuri.
Rangi ya kuchapisha
Chagua rangi ya mhuri.
Uwazi
Chagua iwapo utafanya muhuri iwe wazi au la.
Tarehe ya Mhuri
Tarehe ya Mhuri
Teua Washa ili kuchapisha mihuri ya tarehe kwenye nakala zako.
Umbizo la Tarehe
Teua umbizo la tarehe.
Nafasi ya Stempu
Teua nafasi ta mhuri wa tarehe.
Ukubwa
Teua ukubwa wa mhuri wa tarehe.
Mandhari-nyuma
Teua iwapo unataka kufanya mandharinyuma ya mhuri wa tarehe kuwa rangi nyeupe au la. Iwapo utateua Nyeupe, unaweza kuona mhuri wa tarehe vizuri wakati mandharinyuma ya data sio nyeupe.
Nambari za Kurasa
Nambari za Kurasa
Teua Washa ili kuchapisha nambari za ukurasa kwenye nakala zako.
Umbizo
Teua umbizo la uwekaji nambari kwenye ukurasa.
Nafasi ya Stempu
Teua nafasi ya uwekaji nambari kwenye ukurasa.
Badilisha Nambari
Teua ukurasa unaotaka kuchapisha nambari ya ukurasa. Teua Nambari ya Ukurasa wa Kwanza ili kubainisha ukurasa ambao uchapishaji wa nambari ya ukurasa unafaa kuanza. Pia unaweza kubainisha nambari ya ukurasa inayoanza kwenye Nambari ya Uchapishaji wa Kwanza.
Ukubwa
Teua ukubwa wa nambari.
Mandhari-nyuma
Teua iwapo unataka kufanya mandharinyuma ya nambari ya ukurasa kuwa rangi nyeupe au la. Iwapo utateua Nyeupe, unaweza kuona nambari ya ukurasa vizuri wakati mandharinyuma ya nakala asili sio nyeupe.
Kuhifadhi Faili
Unaweza kuhifadhi taswira iliyotambazwa kwenye hifadhi.
Mpangilio:
Chaguo iwapo utahifadhi taswira iliyotambazwa pekee kwenye hifadhi au la.
Kabrasha (Inahitajika):
Teua hifadhi ambapo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.
Jina la Faili:
Weka jina la faili.
Nenosiri la Faili:
Weka nenosiri ili kuchagua faili.
Jina la Mtumiaji:
Weka jina la mtumiaji.
Seti za Chapisho
Hukuruhusu kuweka mipangilio ya kupanga nakala katika vikundi. Unaweza kuweka idadi ya nakala, idadi ya seti, na chaguo za ukamilisho.
Futa rangi nyekundu
Teua ili kutoa nakala zenye vibambo vyekundu vilivyofutwa kwenye asili.