Kusafisha ADF

Wakati picha zilizonakiliwa au kutambazwa kutoka kwa ADF zimechafuka au za asili haziingii katika ADF ipasavyo, safisha ADF.

Muhimu:

Usiwahi kutumia pombe au thina kusafisha printa. Kemikali hizi zinaweza kuharibu printa.

  1. Fungua kifuniko cha ADF.

  2. Tumia kitambaa safi kilicho na maji kusafisha rola na ndani ya ADF.

    Muhimu:
    • Kutumia kitambaa kilichokauka kunawea kuharibu eneo la rola.

    • Tumia ADF baada ya rola kukauka.

  3. Funga kifuniko cha ADF, na kisha funga kifuniko cha hati.

  4. Safisha sehemu ambayo imeonyeshwa katika kielelezo.

    Rudia kusafisha hadi kusiwe na uchafu wowote.

    Muhimu:
    • Baada ya kusafisha uchafu, pangusa majimaji yote yanayosalia.

    • Iwapo eneo la kioo limekwamiliwa na grisi au nyenzo nyingine ngumu kuondoa, tumia kiasi kidogo cha kisafishaji kioo na kitambaa laini kuiondoa.

    • Usibonyeze glasi kwa nguvu.

    • Kuwa makini usikwaruze au kuharibu glasi. Glasi iliyoharibika inaweza kupunguza ubora wa utambazaji.