Unaweza kuweka nenosiri la msimamizi kwa kutumia Web Config. Unapotumia Web Config, ni muhimu kuunganisha kichapishi kwenye mtandao. Iwapo kichapishi hakijaunganishwa kwenye mtandao, unganisha kwenye kompyuta iliyo na kebo ya Ethaneti moja kwa moja.
Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi
Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.
Chaguo-msingi la User Name ni tupu.
Tazama maelezo husiani hapa chini kwa ajili ya chaguo-msingi la nenosiri la msimamizi.
Teua Log in, na kisha uingize nenosiri la msimamizi, na kubonyeza OK.
Teua Product Security-Change Administrator Password.
Ingiza nenosiri katika Current password na New Password na Confirm New Password. Ingiza jina la mtumiaji, iwapo ni muhimu.
Teua OK.
Ili kurejesha nenosiri la msimamizi kwenye chaguo-msingi lake, chagua Restore Default Settings kwenye skrini ya Change Administrator Password.