Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi
Mipangilio Msingi
Mwangaza wa LCD
Rekebisha mwangaza wa skrini ya LCD.
Sauti
Nyamazisha
Teua On ili kunyamazisha sauti kama zile zitolewazo na Ubonyezaji Kitufe.
Hali ya Kawaida
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe.
Faksi
Teua sauti kwa jili ya utendaji wa faksi unaofuata.
Toni ya Mlio
Weka sauti ya wakati ambapo kichapishi kimepokea faksi.
Pokea Ilani ya Kukamilisha
Weka sauti ya wakati ambapo kupokelewa kwa faksi kumeekamilika.
Chapisha Ilani ya Kukamilisha
Weka sauti ya wakati wa ambapo uchapishaji wa faksi iliyopokelewa umekamilika.
Kipokeaji
Weka sauti ya sauti ya kubofya wakati ambapo kichapishi kinatuma faksi.
Tuma Ilani ya Kukamilisha
Weka sauti ya wakati wa ambapo kutuma faksi kutakamilika.
Ubonyezaji Kitufe
Weka sauti unapodonoa vipengee kwenye skrini katika paneli dhibiti.
Seti ya Nyaraka ya ADF
Weka sauti wakati nakala za kwanza zimewekwa katika ADF.
Ilani ya Ukamilisho
Weka kiwango cha sauti wakati shughuli zimekamilika kwa usahihi.
Mlio wa kosa
Weka sauti wakati kosa linatokea.
Ilani ya Kasoro ya Marudio
Weka ikiwa sauti itarudiwa au kutorudiwa kwa toni ya hitilafu.
Aina ya Sauti
Weka aina ya sauti.
Hali Tulivu
Weka mipangilio ya sauti kwenye Hali Tulivu.
Faksi
Teua sauti kwa jili ya utendaji wa faksi unaofuata.
Toni ya Mlio
Weka sauti ya wakati ambapo kichapishi kimepokea faksi.
Pokea Ilani ya Kukamilisha
Weka sauti ya wakati ambapo kupokelewa kwa faksi kumeekamilika.
Chapisha Ilani ya Kukamilisha
Weka sauti ya wakati wa ambapo uchapishaji wa faksi iliyopokelewa umekamilika.
Kipokeaji
Weka sauti ya sauti ya kubofya wakati ambapo kichapishi kinatuma faksi.
Tuma Ilani ya Kukamilisha
Weka sauti ya wakati wa ambapo kutuma faksi kutakamilika.
Ubonyezaji Kitufe
Weka sauti unapodonoa vipengee kwenye skrini katika paneli dhibiti.
Seti ya Nyaraka ya ADF
Weka sauti wakati nakala za kwanza zimewekwa katika ADF.
Ilani ya Ukamilisho
Weka kiwango cha sauti wakati shughuli zimekamilika kwa usahihi.
Mlio wa kosa
Weka sauti wakati kosa linatokea.
Ilani ya Kasoro ya Marudio
Weka ikiwa sauti itarudiwa au kutorudiwa kwa toni ya hitilafu.
Aina ya Sauti
Weka aina ya sauti.
Kipima saa cha Kulala
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Amsha
Gusa Skrini ya LCD Kuamsha
Teua Washa ili kurudi kutoka kwenye modi ya kulala (modi ya kuhifadhi nishati) kwa kudonoa paneli ya mguso. Wakati imezimwa unahitaji kubonyeza kitufe kilicho kwenye paneli dhibiti ili uamshe printa. Kuzima kipengele hiki huzuia operesheni zozote zisizo kusudiwa zilizosababishwa na vifaa vya nje kugusa skrini. Pia unaweza kuweka kipindi cha muda ambacho kipengele hiki kimewashwa.
Kipima Saa ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Mip'ilio ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha LINE kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Teua mpangilio wa wakati wa majira ya joto unaotumika katika eneo lako.
Utofauti wa Saa
Ingiza tofauti ya saa kati ya saa yako ya ndani na UTC (Saa Inayoratibiwa ya Kimataifa).
Lugha/Language
Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.
Skrini ya Kuanza
Bainisha menyu ya kwanza inayoonyeshwa kwenye skrini ya LCD wakati kichapishi kinawaka na Muda wa Shughuli Umeisha imewezeshwa.
Hariri Ukurasa wa Nyumbani
Badillisha muundo wa ikoni kwenye skrini ya LCD. Pia unaweza kuongeza, kuonmdoa, na kuhamisha ikoni.
Muundo
Teua muundo wa skrini ya nyumbani.
Ongeza Ikoni
Ongeza ikoni kwenye skrini ya mwanzo.
Ondoa Ikoni
Ondoa ikoni kutoka kwa skrini ya mwanzo.
Sogeza Ikoni
Hamisha ikoni kwenye skrini ya mwanzo.
Hatua za Haraka
Unaweza kutumia mpangilio huu iwapo umeongeza ikoni ya njia ya mkato inayopakia uwekaji upya kwa kunakili na kuchanganua kwenye skrini ya nyumbani. Kunakili na kuchanganua huanza mara moja kwa kudonoa tu ikoni ya njia ya mkato kwenye skrini ya nyumbani.
Rejesha Onyesho Msingi la Ikoni
Weka upya uonekanaji wa ikoni za skrini ya nyumbani ili uwe chaguo-msingi.
Muda wa Shughuli Umeisha
Teua On ili kurejesha skrini ya kwanza wakati hakuna operesheni imetekelezwa kwa muda uliobainishwa. Wakati vizuizi vya mtumiaji vimewekwa na hakuna operesheni zinatekelezwa kwa muda uliobainishwa, unaondolewa na kurejeshwa kwenye skrini ya kwanza.
Kibodi
Badillisha muundo wa kibodi kwenye skrini ya LCD.
Skrini chaguo-msingi(Kazi/Hali)
Teua maelezo chaguo-msingi unayotaka kuonyesha unapobonyeza kitufe cha .
Chaguo la Utambuaji Oto wa Ukubwa Asili
Weka kipaumbele kwa Uk. Karat'i Tambua Otomatiki.
ADF na glasi ya kitambazaji zina sensa ambazo hutambua otomatiki ukubwa wa karatasi. Hata hivyo, kutokana na mifano ya sensa, ukubwa sawa hauwezi kutambuliwa, na karatasi ya ukubwa wa K, ambayo inatumika zaidi China, haiwezi kutambuliwa sahihi katika hali ya awali ya kichapishi. Teua Kipaumbele cha Ukubwa wa K iwapo kila mara huwa unatumia ukubwa wa karatasi wa K. Ukubwa asili utatambuliwa kama ukubwa wa K badala ya ukubwa unaokaribia. Kutegemea ukubwa na mwelekeo wa karatasi, inaweza kugunduliwa kama ukubwa mwingine unaokaribia. Pia, ukubwa wa K unaweza kukosa kugunduliwa kutegemea kazi unayotumia. Kwa mfano, unapotambaza na kuhifadhi kwenye kompyuta kwa kutumia programu hiyo, kama au la ukubwa wa K unaweza kutambuliwa otomatiki kunategemea tabia ya programu hiyo.