> Katika Hali Hizi > Kuhamisha na Kusafirisha Kichapishi > Kuandaa Kuhamisha Kichapishi

Kuandaa Kuhamisha Kichapishi

  1. Zima kichapishi kwa kubonyeza kitufe cha .

  2. Hakikisha taa ya nishati imezima, na kisha uchomoe waya ya nishati.

    Muhimu:

    Chomoa waya ya nishati wakati taa ya nishati imezimwa. La sivyo, kichwa cha kuchapisha hakitarudi kwenye mkao wake na wino utakauka, na huenda isiweze kuchapisha.

  3. Tenganisha kebo zote kama vile waya ya nishati na kebo ya USB.

  4. Iwapo kichapishi huauni vifaa vya hifadhi ya nje, hakikisha havijaunganishwa.

  5. Ondoa trei towe.

    Tahadhari:

    Uwiweke trei towe iliyoondolewa kwenye kichapishi kwa kuwa sio imara. Iwapo trei towe itaanguka kichapishi kinapohamishwa unaweza kujeruhiwa.

  6. Ondoa karatasi zote kutoka kwa kichapishi.

  7. Hakikisha hakuna nakala za kwanza kwenye kichapishi.

  8. Hifadhi auni ya karatasi.

Kichapishi kiko tayari kusogezwa.

Angalia Maelezo Husiani iwapo unasakinisha vipengee vyovyote vya hiari.