Ubora wa Taswira ya Faksi Iliyotumwa ni Duni

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Mpangilio wa Aina ya Nakala Asili sio sahihi.

Suluhisho

Teua Faksi > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Utambazaji > Aina Asili, na kisha ubadilishe mpangilio. Iwapo nakala asili unayotuma ina matini na taswira, weka hii iwe Picha.

Mwonekano umewekwa kuwa chini.

Suluhisho

Iwapo hufahamu utendaji wa mashine ya faksi ya mtumaji, weka yafuatayo kabla ya kutuma faksi.

  • Teua Faksi > Mipangilio ya Faksi na kisha uweke mpangilio wa Mwonekano ili uweke taswira ya ubora wa juu zaidi.

  • Teua Faksi > Mipangilio ya Faksi na kisha uwezeshe Tuma Moja kwa Moja.

    Kumbuka kwamba ukiweka Mwonekano iwe Bora Zaidi au Bora Sana lakini utume faksi bila kuwezesha Tuma Moja kwa Moja, faksi inaweza kutumwa kwa ubainifu wa chini.

Ubora wa Picha wa Faksi Zilizotumwa Haukuwi Bora Baada ya Kujaribu Suluhisho za Hapa Juu

Suluhisho

Ikiwa huwezi kutatua shida hiyo, wasiliana na msimamizi wako wa kichapishi. Kwa wasimamizi wa kichapishi, tazama sehemu inayofuata ili kutatua matatizo ya faksi.

Ubora wa Faksi Iliyotumwa au Iliyopokelewa ni Duni