Katika hali zifuatazo, leta CA Certificate kwenye kichapishi.
Tumia IEEE802.1X (Wi-Fi)
Certificate Validation ukitumia IEEE802.1X (Wired LAN)
Halalisha IPsec/IP Filtering kwa cheti.
Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya mtandao (kamili/wa ziada) ambao unataka kusanidi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani au Ya Ziada) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi
Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.
Teua kwenye orodha inayofuata.
Kichupo cha Network Security > CA Certificate
Bofya Import.
Bainisha CA Certificate unachotaka kuleta.
Bofya OK.
Ukikamilisha kuleta, unaweza kurejea kwenye skrini ya CA Certificate, na CA Certificate kilicholetwa kinaonyeshwa.