Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.
Onyesha Mipangilio/Ficha Mipangilio
Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.
Rejesha Chaguo-msingi
Rejesha mipangilio yote katika thamani chaguomsingi za kiwanda. Mipangilio kwenye kichupo cha Kuu pia hurejeshwa katika chaguomsingi zao.
Aina ya Uchapishaji
Teua Kazi ya Siri ili uweke nenosiri la kulinda nyaraka za siri unapochapisha. Iwapo utatumia kipengele hiki, data ya kuchapisha inahifadhiwa kwenye kichapishi na inaweza kuchapishwa tu baada ya nenosiri kuingizwa kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi. Bofya Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.
Usahihishaji wa Rangi
Otomatiki
Hurekebisha rangi za picha kiotomatiki.
Kaida
Hukuruhusu ili kutekeleza urekebishaji wa rangi kikuli. Kubofya Iliyoboreshwa hufungua skrini ya Usahihishaji wa Rangi ambapo unaweza kuchagua mbinu ya kina ya urekebishaji wa rangi. Hukuruhusu kuweka mbinu ya Chapisho Lote la Rangi ili kukoleza matini na mistari unapobofya Chaguo za Taswira. Unaweza pia kuwezesha Ula'aji wa Pambizo na Rkbsha Jicho Jekundu.
Mipangilio ya Ziada
Vipengele vya Taswira fifi
Hukuruhusu kuunda mipangilio kwa ruwaza za kutonakili, taswira fifi, au vijajuu na vijachini.
Ongeza/Futa
Hukuruhusu kuongeza au kuondoa ruwaza zozote za kutonakili na nakala au taswira fifi unazotaka kutumia.
Mipangilio
Hukuruhusu kuweka mbinu ya uchapishaji kwa ruwaza za kutonakili au taswira fifi.
Kijajuu/Kijachini
Unaweza kuchapisha maelezo kama vile jina la mtumiaji na tarehe ya kuchapisha kwenye vijajuu na vijachini.
Zungusha 180°
Huzungusha kurasa nyuzi 180 kabla ya kuchapisha. Teua kipengee hiki unapochapisha kwenye karatasi kama vile bahasha zilizopakiwa katika mwelekeo thabiti kwenye kichapishi.
Uchapishaji katika mielekeo miwili
Huchapisha wakati kichwa cha kuchapisha kinasogea pande zote mbili. Kasi ya uchapishaji na haraka, lakini ubora unaweza kupungua.
Taswira ya Kioo
Hugeuza picha ili iweze kuchapisha kama vile ingeonekana kwenye kioo.
Modi Tulivu
Hupunguza kelele ambayo kicvhapishi hutoa. Hata hivyo, uwezeshaji wa hii unaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.