Kutoka kwenye kompyuta, unaweza kuandika au kusoma data kwenye kifaa cha kumbukumbu kama vile kifaa cha USB ambacho ikmechomekwa kwenye kichapishi.
Unaposhiriki kifaa cha kumbukumbu kilichochomekwa kwenye kichapishi kati ya kompyuta iliyounganishwa na USB au kupitia mtandao, haki ya ufikiaji imeruhusiwa tu kwa kompyuta zimeunganishwa kupitia mbinu ambayo uliteua kwenye kichapishi. Ili kuandika kwenye kifaa cha kumbukumbu, weka Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Kiolesura cha Kifaa cha Kumbukumbu > Kushiriki Faili kwenye paneli dhibiti kisha uteue njia ya muunganisho.
Huchukua muda ili kutambua data kutoka katika kompyuta ikiwa kifaa kikubwa cha kumbukumbu kama vile TB 2 HDD kimeunganishwa.
Teua kifaa cha kumbukumbu kutoka PC au Kopmyuta. Data kwenye kifaa cha kumbukumbu inaonyeshwa.
Iwapo umeunganisha kichapishi kwenye mtandao bila kutumia kisakinishaji, ramanisha kituo tayarishi cha USB kama kiendeshi cha mtandao. Fungua Endesha na uingize jina la kichapishi \\XXXXX au anwani ya IP ya kichapishi \\XXX.XXX.XXX.XXX ili Fungua:. Bofya kulia kwenye ikoni ya kifaa iliyoonyeshwa ili upangie mtandao. Kiendeshi cha mtandao hutokea katika PC au Kompyuta.
Teua ikoni inayolingana ya kifaa. Data kwenye kifaa cha hifadhi ya nje inaonyeshwa.
Ili kuondoa kifaa cha kumbukumbu, buruta na udondoshe aikoni ya kifaa kwenye aikoni ya tupio. Vinginevyo, huenda data kwenye hifadhi ya pamoja isionyeshwe ipasavyo wakati kifaa kingine cha kumbukumbu kimechomekwa.
Ili kufikia kifaa cha kumbukumbu kupitia mtandao, teua, Nenda > Unganisha kwenye Seva kutoka katika menyu kwenye eneo-kazi. Ingiza jina la kichapishi cifs://XXXXX au smb://XXXXX (Ambapo “XXXXX” ni jina la kichapishi) katika Anwani ya Seva, na kisha ubofye Unganisha.