Unaweza kupunguza au kuongeza ukubwa wa hati na asilimia mahsusi.

Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi Kuu, teua ukubwa wa waraka kutoka kwenye mpangilio wa Ukubwa wa Waraka.
Teua ukubwa wa karatasi unaotaka kuchapisha kutoka kwenye mpangilio wa Karatasi ya Zao.
Chagua Kuza hadi, na kisha uandike aslimia. Iwapo umeteua Sawa na Ukubwa wa Waraka kama Karatasi ya Zao, teua Punguza/Kuza Waraka kwanza.
Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.
Bofya Chapisha.