Unaweza kukatiza kazi ya sasa ya kuchapisha na kutekeleza kazi nyingine iliyopokewa.
Hata hivyo, huwezi kukatiza kazi mpya kutoka kwenye kompyuta.
Bonyeza kitufe cha
kwenye paneli dhibiti ya kichapishi unapochapisha.
Uchapishaji unakatizwa na kichapishi kinaingia modi ya ukatizaji.
Teua Hali ya Kazi kwenye skrini ya nyumbani.
Teua kichupo cha Kazi, kisha uteue kazi unayotaka kukatiza kutoka kwenye orodha ya Inatumika.
Teua Maelezo ili kuonyesha Maelezo ya Kazi.
Teua Katiza kwenye skrini iliyoonyeshwa.
Kazi ya kuchapisha uliyoteua imetekelezwa.
Ili kuwasha upya kazi iliyositishwa, bonyeza kitufe cha
tena ili kutoka kwenye modi ya ukatizaji. Pia, wakati hakuna operesheni zinazotekelezwa kwa kipindi kirefu maalum cha muda baada ya ukatizaji wa kazi ya kuchapisha, kichapishi kinatoka kwenye modi ya ukatizaji.