Kukagua na Kusafisha Kichwa cha Kuchapisha

Ikiwa nozeli zimeziba, uchapishaji unakuwa fifu, mistati inaonekana, au rangi zisizotarajiwa zinaonekana. Ikiwa nozeli zimeziba sana, karatasi tupu itachapishwa. Wakati ubora wa chapisho umepungua, kwanza tumia kipengele cha kukagua nozeli na ukague kama nozeli zimeziba. Ikiwa nozeli zimeziba, safisha kichwa cha kuchapisha.

Muhimu:
  • Usifungue kifuniko cha kitengo cha kutoa wino au kuzima kichapishi wakati wa kusafisha kichwa. Ikiwa usafisha wa kichwa haujakamilika, huenda usiweze kuchapisha.

  • Kwa kuwa usafishaji wa kichwa cha chapisho hutumia wino kiasi, unaweza kutekelezwa wakati wino umepungua.

  • Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kurudia kuangalia nozeli na kusafisha kichwa mara 4, subiri kwa angalau saa 6 bila kuchapisha, angalia nozeli tena , na kisha urudie usafishaji wa kichwa ikiwa ni muhimu. Tunapendekeza uzime kichapishi kwa kutumia kitufe cha . Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujaimarika, endesha Usafishaji wa Nishati.

  • Ili kuzuia kichwa cha kuchapisha kisikaue, usichomoe printa wakati nishati imewashwa.

Unaweza kuangalia na kusafisha kichwa cha kuchapisha kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi.

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua Matengenezo > Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa.

  3. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini kuchapisha ruwaza ya kukagua nozeli.

  4. Angalia ruwaza iliyochapishwa ili kuona iwapo nozeli za kichwa cha kuchapisha zimezibika.

    • A:
      Mistari yote imechapishwa. Teua . Hakuna hatua za ziada zinazohitajika.
    • B au karibu na B
      Baaadhi ya nozeli zimeziba. Teua , kisha uteue Usafishaji Kichwa cha Chapa kwenye skrini inayofuata.
    • C au karibu na C
      Iiwa laini nyingi hazipo au hazijachapishwa, hii inaonyesha kwamba nozeli nyingi zimeziba. Endesha Usafishaji wa Nishati.
  5. Wakati Usafishaji Kichwa cha Chapa umekamilika, chapisha tena ruwaza ya nozeli ya kagua. Rudia usafishaji na uchapishaji hadi mistari yote ichapishwe kabisa.