Soma maagizo yafuatayo kabla ya kubadilisha kisanduku cha ukarabati.
Usiguse chipu ya kijani iliyo upande wa kando wa kisanduku cha ukarabati. Kufanya hivyo kunaweza kuzuia utendaji na uchapishaji wa kawaida.
Usiondoe utepe uliojuu ya kisanduku; la sivyo wino unaweza kuvuja.
Usiinamishe kisanduku cha ukarabati kilichotumiwa hadi kifungiwe ndani ya mfuko wa plastiki; la sivyo wino unaweza kuvuja.
Weka kisanduku cha ukarabati mbali na mwale wa jua wa moja kwa moja.
Usihifadhi kisanduku cha ukarabati katika halijoto za juu au zinazoganda.
Usibadilishe kisanduku cha ukarabati wakati wa uchapishaji; la sivyo, wino unaweza kuvuja.
Usitumie upya kisanduku cha ukarabati ambacho kimeondokewa na kutotumiwa kwa muda mrefu. Wino ndani ya kisanduku hicho umekauka na hakuna wino zaidi unaweza kunyonywa.