EPSON Software Updater ni programu ambayo husakinisha programu mpya na kusasisha vifaa dhabiti na miongozo kupitia Mtandao. Iwapo unataka kuangalia taarifa ya visasisho mara kwa mara, unaweza kuweka kipindi cha kuangalia visasisho kwenye Mipangilio ya EPSON Software Updater ya Sasisho Otomatiki.
Programu endeshi za Windows Server hazikubaliwi.
Kwa watumiaji katika Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kilatini: kichapishi chako kimebuniwa kufanya kazi tu na vibweta halisi vya wino vya aina ya Epson. Aina nyingine za vitengo vya vifaa vya wino na vifaa vya wino havitangamani na, hata ikiwa imeelezewa kuwa vinatangamana, huenda visifanye kazi vizuri au visifanye kamwe. Epson hutoa masasisho ya programu msingi mara kwa mara ili kushughulikia matatizo ya usalama, utendaji, urekebishaji tatizo ndogo na kuhakikisha kichapishi kinafanya kazi kama kilivyobuniwa. Masasisho haya huenda yakaathiri utendakazi wa wino ya mhusika mwingine. Vitengo vya vifaa vya wino vilivyoingiliwa au visivyo vya aina ya Epson ambavyo vilifanya kazi kabla ya sasisho la programu msingi huenda visiendelee kufanya kazi.
Windows 11
Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu zote > EPSON Software > Epson Software Updater.
Windows 10
Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue EPSON Software > Epson Software Updater.
Windows 8.1/Windows 8
Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.
Windows 7
Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote (au Programu) > EPSON Software > Epson Software Updater.
Kadhalika, unaweza kuwasha EPSON Software Updater kwa kubofya ikoni ya kichapishi kwenye mwambaa kazi ulio kwenye eneo kazi, na kisha uteue Kisasisho cha Programu.
Teua Nenda > Programu > Epson Software > EPSON Software Updater.