Kutuma Faksi kwa Kutumia Seva ya Faksi

Unaweza kutuma faksi kwa kutumia seva ya faksi kwenye mtndao wako. Kusanidi seva ya faksi hukuruhusu utume baruapepe kwenye seva ya faksi ukiwa umeambatisha data ya faksi, na kisha uitume ukitumia kipengele cha faksi cha kichapishi. Seva ya faksi hutuma faksi kwa kutumia nambari ya faksi ya mpokeaji ikijumuisha anwani ya baruapepe. Wakati mipangilio ya seva ya faksi imewezeshwa, hauwezi kutuma faksi kwa kutumia kituo cha LINE kwenye kichapishi.

Kumbuka:

Kabla ya kuleta kipengele hiki kwenye mtandao wako, shauriana na mwakilishi wa mauzo ili kupata maelezo zaidi. Ili kupata maelezo kwenye seva ya faksi, shauriana na mtoa huduma kwa ajili ya faksi za Intaneti.

A: Seva ya faksi

B: Mtandao wa Simu Uliobadilishwa wa Umma (PSTN)

C: Baruapepe pamoja na data ya faksi imeambatishwa

Unahitaji seva ya faksi iliyo na vipengele vifuatavyo.
  • Uwezo wa kupokea data ya faksi na baruapepe katika umbizo la "XXXXXX@YYYYYY", na utume faksi kwenye nambari ya faksi XXXXXX

    XXXXXX: Nambari ya faksi

    YYYYYY: Jina la miliki la seva ya faksi lililoongezwa na kichapishi

  • Uwezo wa kushughulikia data ya faksi ya umbizo la multi- Tiff iliyoambatishwa kwenye baruapepe