> Mwongozo wa Paneli Dhibiti > Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Hii huonyeshwa wakati programu msingi inapatikana.

Donoa ili kusasisha programu maunzi ili kuboresha vipengele vya kichapishi. Tunapendekeza kutumia kichapishi na toleo la hivi karibuni zaidi la programu maunzi.

Huonyesha skrini ya Hali ya Printa.

Unaweza kuangalia kiwango cha wino na kiwango cha maisha ya huduma ya kikasha cha ukarabati.

Huonyesha hali ya muunganisho wa mtandao. Angalia yafuatayo kwa maelezo zaidi.

Mwongozo kwa Aikoni ya Mtandao

Huonyesha skrini ya Mipangilio ya Sauti ya Kifaa.

Unaweza kuweka Nyamazisha na Hali Tulivu. Unaweza kufikia menyu ya Sauti kutoka kwenye skrini.

Huonyesha iwapo Hali Tulivu imewekwa klwa kichapishi au la. Kipengele kinapowezeshwa, kelele iliyopigwa na operesheni za kichapishi inapunguika, lakini kasi ya kuchapisha inaweza kupungua. Hata hivyo, huenda kelele isipungue kwenye aina ya karatasi iliyoteuliwa na ubora wa chapisho.

Huonyesha kuwa Nyamazisha imewekwa kwa kichapishi.

Teua ikoni ili kuingiza modi ya kusinzia. Wakati ikoni imewekewa rangi ya kijivu, kichapishi hakiwezi kuingiza modi ya kusinzia.

Huonyesha kuwa kipengele cha kizuizi cha mtumiaji kimewezeshwa. Teua ikoni hii ili kuingia kwenye kichapishi. Unahitaji kuteua jina la mtumiaji na kisha ingiza nywila. Wasiliana na msimamizi wako wa kichapishi kwa maelezo ya kuingia.

Wakati imeonyeshwa, mtumiaji aliye ya idhini ya ufikiaji ameingia. Teua aikoni ili uondoke.

Huonyesha skrini ya Maelezo ya Data ya Faksi. Nambari inayoonyeshwa inaashiria idadi ya faksi ambazo bado hujasoma, kuchapisha au kuhifadhi.

Huonyesha kila menyu.

  • Nakili

    Hukuruhusu kunakili nyaraka.

  • Faksi

    Hukuruhusu kutuma faksi.

  • Changanua

    Hukuruhusu kutambaza nyaraka na kuzihifadhi kwenye kifaa cha kumbukumbu au kompyuta.

  • Zili'a Kabla

    Hukuruhusu kusajili mipangilio inayotumika mara kwa mara kunakili, kutambaza au kutuma faksi kama uwekaji awali.

    Baada ya kusajili, unaweza kuongeza ikoni ya njia ya mkato kwenye skrini ya mwanzo ambayo hupakia iliyowekwa mapema. Kwa ajili ya kunakili na kuchanganua zilizowekwa mapema, unaweza kusanidi ikoni ya njia ya mkato ili kuanza mara moja kwa kugusa ikoni ya njia ya mkato.

  • Kifaa cha Kumbukumbu

    Hukuruhusu kuchapisha data ya JPEG, TIFF au PDF kwenye kifaa cha kumbukumbu kama vile kifaa cha kumbukumbu cha USB kilichounganishwa kwenye kichapishi.

  • Kasha la Faksi

    Hukuruhusu kuhifadhi hati zilizopokelewa, hati za kutuma au hati kwa ajili ya kutuma faksi.

  • Chapisha Kutoka Kumb'u Ndani

    Hukuruhusu kuhifadhi kazi zilizotumwa kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi hadi kwenye kumbukumbu ya kichapishi kwa muda kabla ya kuchapisha. Unaweza kuchapisha kazi iliyolindwa kwa nenosiri na kuweka machapisho ya jaribio unapochapisha nakala nyingi.

  • Mipangilio

    Hukuruhusu kuweka mipangilio inayohusiana na udumishaji, mipangilio ya kichapishi na operesheni.

Kazi/Hali

Huonyesha kazi zinazoendelea zinazosubiri. Donoa ili kuonyesha aina ya kazi, kipima muda wa kuwasili, majina ya mtumiaji, nakadhalika kama orodha. Nambari inayoonyeshwa huashiria idadi ya kazi zinazosubiri.

Hutelezesha skrini upande wa kulia.