Unapowezesha udhibiti wa ufikiaji, mtumiaji aliyesajiliwa pekee ndiye ataweza kutumia kichapishi.
Wakati Access Control Settings imewezeshwa, unahitaji kuarifu mtumiaji kuhusu maelezo ya akaunti yao.
Unapochapisha kutoka kwenye kompyuta, weka maelezo ya mtumiaji wa kichapishi kwenye kompyuta ya mteja.
Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.
Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.
Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi
Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.
Teua kwenye orodha inayofuata.
Kichupo cha Product Security > Access Control Settings > Basic
Teua Enables Access Control.
Ukiwezesha Udhibiti wa Ufikiaji na unataka kuchapisha au kutambaza vifaa mahiri ambavyo havina maelezo ya uhalalishaji, teua Allow printing and scanning without authentication information from a computer.
Kiendeshi cha kichapishi cha Windows cha Epson hukuruhusu kuweka maelezo ya mtumiaji mapama. Kwenye Mac OS, unahitaji kuingiza maelezo ya mtumiaji kila wakati unachapisha.
Bofya OK.
Ujumbe wa ukamilisho unaonyeshwa baada ya muda fulani.
Thibitisha kwamba ikoni kama vile nakili na utambaze zimelemazwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.