> Katika Hali Hizi > Kusakinisha au Kuondoa Programu Kando > Kusakinisha Programu Kando > Kukagua ikiwa kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson kimesakinishwa — Windows

Kukagua ikiwa kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson kimesakinishwa — Windows

Unaweza kuangalia iwapo kiendeshi halali cha kichapishi cha Epson kimesakinishwa kwenye kompyuta yako kwa kutumia mojawapo ya mbinu zifuatazo.

  • Windows 11

    Bofya kwenye kitufe cha kuanza, na kisha uteue Mipangilio > Bluetooth na vifaa > Vichapishi na vichanganuzi, na kisha ubofye Chapisha sifa za seva chini ya Mipangilio husika.

  • Windows 10/Windows 8.1/Windows 8/Windows 7/Windows Server 2022/Windows Server 2019/Windows Server 2016/Windows Server 2012 R2/Windows Server 2012/Windows Server 2008 R2

    Teua Paneli Dhibiti > Ona vifaa na vishapishi (Vichapishi, Vichapishi na Faksi) ndani ya Maunzi na Sauti, bofya ikoni ya kichapishi, na kisha ubofye Sifa za sevaya uchapishaji katika upande wa juu wa dirisha.

  • Windows Server 2008

    Bofya kulia kwenye kabrasha la Vichapishi, na kisha ubofye Endesha kama msimamizi > Sifa za Seva.

Bofya kichupo cha Viendeshi. Iwapo jina la kichapishi chako litaonyeshwa kwenye orodha, kiendeshi halali cha Epson kimesakinishwa kwenye kompyuta yako.