> Maelezo ya Msimamizi > Kudhibiti Kichapishi > Mipangilio ya Uokoaji wa Nishati wakati wa Kutotumika

Mipangilio ya Uokoaji wa Nishati wakati wa Kutotumika

Unaweza kuweka muda wa kubadilika hadi hali ya uokoaji nishati au kuzima nishati wakati paneli dhibiti ya kichapishi hakitumiki kwa kipindi fulani cha wakati. Weka muda kulingana na mazingira yako ya matumizi.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Device Management > Power Saving

  4. Weka vipengee vifuatavyo inavyohitajika.

    • Sleep Timer
      Ingiza muda wa kubadili hadi hali ya uokoaji nishati wakati hakitumiki.
    Kumbuka:

    Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Kipima saa cha Kulala

    • Power Off Timer au Power Off If Inactive
      Teua muda kutoka wakati kichapishi hakijakuwa amilifu hadi wakati kinazima kiotomatiki. Unapotumia vipengele vya faksi, teua None au Off.
    Kumbuka:

    Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Kipima Saa ya Kuzima au Mip'ilio ya Kuzima > Zima Ikiwa Haitumiki

    • Power Off If Disconnected
      Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi baada ya kipindi cha muda uliobainishwa wakati vituo tarishi vyote vinajumuisha kituo tayarishi cha LINE vimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
      Tazama tovuti inayofuata ili kupata kipindi cha muda uliobainishwa.
    Kumbuka:

    Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Mip'ilio ya Kuzima > Zima ikiwa Imetenganishwa

    • Wake with LCD Screen Touch
      Unaweza kuweka jinsi ambavyo paneli ya mguso inavyojiwashwa kutoka kwenye modi ya kusinzia. Iwapo utateua Schedule, weka muda wa kuanza na kuisha kwa modi ya kusinzia.
    Kumbuka:

    Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Amsha > Gusa Skrini ya LCD Kuamsha

  5. Bofya OK.