Kusanidi Cheti kwa ajili ya S/MIME

Sanidi cheti cha mteja ili kutumia kitendaji cha cheti cha S/MIME.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya mtandao (kamili/wa ziada) ambao unataka kusanidi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > (Wastani au Ya Ziada) > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Network Security > S/MIME > Client Certificate

  4. Bainisha cheti cha kutumia katika Client Certificate.

    • Self-signed Certificate
      Cheti cha kujitilia sahihi mwenyewe kimezalishwa na kichapishi, unaweza kuteua hiki.
    • CA-signed Certificate
      Ukipokea na kuleya cheti kilichotiwa sahihi na CA mapema, unaweza kubainisha hili.
  5. Bofya Next.

    Ujumbe wa uthibitishaji unaonyeshwa.

  6. Bofya OK.

    Kichapishi kimesasishwa.