Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.
Tunapendekeza uangalie hali ya kichapishi kwenye Hali ya Kazi, iwapo kichapishi kwa sasa kinapokea faksi au la.
Suluhisho
Nyaraka 200 zilizopokewa zimehifadhiwa kwenye kikasha pokezi na kikasha cha siri kwa jumla. Futa nyaraka zisizofaa.
Suluhisho
Faksi zilizotumwa kutoka kwenye nambari ambazo hazijasajiliwa kwenye orodha ya waasiliani zimewekwa ili kuzuiwa. Sajili nambari ya faksi ya mtumaji kwenye orodha ya mwasiliani.
Suluhisho
Faksi ambazo hazina maelezo ya kijajuu zitazuiliwa. Uliza mtumaji iwapo maelezo yamesanidiwa kwenye mashine yake ya faksi.
Suluhisho
Wakati umeunda mipangilio ya kuhifadhi faksi zilizopokewa kwenye kompyuta, washa kompyuta. Faksi iliyopokewa itafutwa pindi tu imehifadhiwa kwenye kompyuta.
Suluhisho
Unapopokea faksi kutumia kipengele cha anwani ndogo, thibitisha kuwa anwani ndogo na nywila ni sahihi. Thibitisha na mtumaji kuwa anwani ndogo na nywila zinalingana.