Tumia huduma ya wingu ya Epson, Epson Connect kutuma picha zilizotambazwa kwa mafikio yaliyosajiliwa.
Unaweza kutuma picha zilizotambazwa kwa urahisi kupitia barua pepe kwa kusajili anwani ya barua pepe kama ufikio.
Unaweza kutuma picha zilizotambazwa kwa huduma za hifadhi ya mtandaoni za mhusika mwingine kwa kuzisajili kama ufikio. Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kusajili akaunti, tazama tovuti kwa kila huduma. Huduma zinazopatikana zinaweza kubadilishwa bila ilani.
Kewa maelezo zaidi kuhusu huduma za Epson Connect, tembelea tovuti ifuatayo ya kituo tayarishi.
http://www.epsonconnect.eu (Ulaya peke yake)
|
Operesheni Muhimu |
Eneo la Operesheni |
Fafanuzi |
|---|---|---|
|
1. Unganisha kichapishi kwenye mtandao (Hii ni umuhimu iwapo uliunganisha kwenye usanidi wakati wa mtandao) |
Kichapishi na kompyuta |
Unganisha printa kwenye mtandao. |
|
2. Sajili bidhaa kwa Epson Connect |
Paneli dhibiti ya kichapishi na kompyuta (Tovuti ya Epson Connect) |
Sajili bidhaa yako kwa Epson Connect na uwezeshe huduma. Kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Huduma ya Wavuti, na kisha ufuate maagizo ya kwenye skrini Ili kujisajili. Iwapo utaombwa kuingiza msimbo wa uthibitishaji, fikia URL ifuatayo na uingize msimbo. |
|
3. Sajili orodha ya ufikio kwenye ukurasa wa mtumiaji wa Epson Connect |
Kompyuta (Tovuti ya Epson Connect) |
Sajili mafikio unayotaka kutuma kwenye orodha ya ufikio kwenye ukurasa wa mtumiaji wa Epson Connect. Fikia ukurasa wa mtumiaji kutoka kwenye URL ifuatayo, bofya Tambaza kwa Wingu > Orodha ya Ufikio > Ongeza*, na kisha ufuate maagizo ya kwenye skrini. Ili kuongeza ufikio. https://www.epsonconnect.com/user Wakati unasajili anwani ya barua pepe, teua Anwani ya Barua pepe kama aina ya ufikio. |
|
4. Changanua kutoka kwenye paneli dhibiti |
Paneli dhibiti ya kichapishi |
Unapochanganua kutoka kwenye peneli dhibiti. |
* Huduma za Epson Connect zinaweza kubadilishwa bila ilani.