Suluhisho
Lainisha kichwa cha kuchapisha kwa kutumia kipengele cha Urekebishaji wa Ubora wa Chapa.
Suluhisho
Ikiwa ubora wa chapisho hautaimarika hata baada ya kulinganisha kichwa, lemaza mpangilio wa uchapishaji wa pande mbili.
Wakati wa uchapishaji wa pande mbili (au kasi ya juu), kichwa cha kuchapisha huchapisha kikisogea pande zote mbili, na mistari wima huenda ikakosa kulingana. Kulemaza mipangilio huenda kukapunguza kasi ya uchapishaji lakini kukaimarisha ubora wa chapisho.
Teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa, kisha ulemaze Mwelekeo kwenye paneli dhibiti.
Suluhisho
Unapotumia ADF
Usiweke nakala asili kwenye ADF. Weka nakala asili kwenye glasi ya kitambazaji badala yake.
Unapotumia glasi za kitambazaji
Lainisha mikunjo na kukunjama kwenye nakala asili kadri iwezekanavyo. Unapoweka nakala asili, jaribu kuweka kipande cha kadi na kadhalika juu ya waraka ili isiinuke, na isalie kulandana karibu na eneo.