> Kutuma Faksi > Kupokea Faksi kwenye Kichapishi

Kupokea Faksi kwenye Kichapishi

Iwapo kichapishi kimeunganishwa kwenye laini ya simu na mipangilio msingi imekamilishwa kwa kutumia Sogora ya Mpangilio wa faksi, unaweza kupoklea faksi.

Unweza kuhifadhi faksi zilizopokewa, kuzikagua kwenye skrini ya kichapishi, na kuzisambaza.

Faksi zilizopokewa zinachapishwa kwenye mipangilio ya kwanza ya kichapishi.

Unapotaka kukagua hali ya mipangilio ya faksi, chapisha Mipangilio ya Orodha ya Faksi kwa kuteua Faksi > (Zaidi) > Ripoti ya Faksi > Mipangilio ya Orodha ya Faksi.

Kumbuka:
  • Hauwezi kufanya yafuatayo huku unapokea faksi.

    - Pokea faksi zingine sawia kwenye mstari mmoja

    - Tuma faksi kwenye mstari mmoja

  • Unaweza kutekeleza shughuli za kutuma faksi (hadi kwenye awamu ya kuhifadhi kazi) hata unapopokea faksi.

    Hata hivyo, hauwezi kutekeleza shughuli za kutuma faksi kwa kazi ambazo haziwezi kuhifadhiwa, kama vile kutuma ukitumia Kw. Kiopoo au Tuma Moja kwa Moja.