Unaweza kuangalia takriban ya viwango vya wino na maisha ya huduma ya kikasha cha matengenezo kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Chagua
kwenye skrini ya mwanzo.
Yafuatayo yanaashiria kiasi cha nafasi tupu katika kikasha cha matengenezo.
A:Nafasi tupu
B:Kiasi cha wino la taka

Unaweza kuendelea kuchapisha wakati ujumbe wa kupungua kwa wino umeonyeshwa. Badilisha vitengo vya kutoa wino kinapohitajika.
Pia unaweza kuangalia makadirio ya viwango vya wino na makadirio ya maisha ya huduma ya kisanduku cha matengenezo kutoka kwenye kiwambo cha hali kwewnye kiendeshi cha kichapishi. Kwa watumiaji wa Windows, kumbuka kuwa unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuwezesha kipengele hiki.
Windows
Bofya EPSON Status Monitor 3 kwenye kichupo cha Utunzaji.
Ikiwa EPSON Status Monitor 3 imelemazwa, bofya Mipangilio Iliyorefushwa kwenye kichupo cha Utunzaji, na kisha uteue Wezesha EPSON Status Monitor 3.
Mac OS
Apple menyu > Mapendeleo ya Mfumo > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi) > Epson(XXXX) > Chaguo na Usambazaji > Matumizi > Fungua Matumizi ya Kichapishaji > EPSON Status Monitor