Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili
Kurasa Nyingi
Teua muundo wa nakala.
Ukurasa Mmoja
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.
2-juu
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.
4-juu
Hunakili hati halisi zenye pande nne kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 4-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.
Ukubwa Asili
Chagua ukubwa wa nakala yako ya kwanza. Unapoteua Tambua Otomatiki, ukubwa wa nakala yako asili inagunduliwa kiotomatiki. Unaponakili nakala asili zisizo za ukubwa wa kawaida, teua Iliyofasiliwa na Mtumiaji, kisha ubainishe ukubwa asili.
Kumalizia
Teua jinsi ya kuondoa karatasi kwa nakala anuwai za hati halisi anuwai.
Kikundi (Kurasa Sawa)
Hunakili nakala asili kwa ukurasa kama kikundi.
Pangiliza (Mpang'o wa Ukurasa)
Huchapisha nakala nyingi za hati nyingi halisi zilizolinganishwa kimpangilio na kupangwa kwenye vikundi.
Kijitabu
Bainisha mipangilio hii unapotaka kuunda kijitabu kutoka kwenye nakala zako.
Kijitabu
Hukuruhusu kuunda kijitabu kutoka kwenye nakala zako.
Kufunga
Teua nafasi ya uunganishaji wa kijitabu.
Pambizo ya Ufungaji
Teua ukingo wa kuunganisha. Unaweza kuweka 0 hadi 50 mm kuwa ukingo wa uunganishaji kwa uongenezaji wa 1 mm.
Jalada
Hukuruhusu kuongeza majalada kwenye kijitabu.
Ukubwa Asili
Chagua ukubwa wa nakala yako ya kwanza.
Mipangilio ya K'si
Teua chanzo cha karatasi unachotaka kutumia ili kuchapisha.
Pande 2
Teua muundo wa pande 2.
Na. Asili zina Mch'o
Unaweza kuweka mchanganyiko ufuatao wa ukubwa kwenye ADF kwa wakati mmoja. A3 na A4; B4 na B5. Unapotumia michanganyiko hii, nakala asili zinanakiliwa kwa ukubwa halisi wa nakala asili. Weka nakala zako asili kwa kupanga upana wa nakala asili kama ilivyoonyeshwa hapa chini.
Mwelekeo (Asili)
Teua mwelekeo wa nakala yako asili.
Kitabu →Kurasa2
Hunakili kurasa zenye pande mbili za kijitabu kwenye karatasi ya kando ya karatasi.
Teua ukurasa wa kijitabu wa kutambaza.
Endelea Kutambaza
Unaweza kuweka idadi kubwa ya nakala asili kwenye ADF katika bechi, na kuzitambaza kama kazi moja ya utambazaji.
Ubora wa Taswira
Rekebisha mipangilio ya taswira.
Ulinganuzi
Rekebisha tofauti kati ya mwangaza na sehemu za giza.
Kulowesha
Rekebisha udhahiri wa rangi.
Uwiano Mwekundu, Uwiano wa Kijani, Uwiano wa Bluu
Rekebisha wiani wa kila rangi.
Ukali
Rekebisha ufupisho wa taswira.
Udhibiti wa Rangi
Rekebisha toni ya rangi ya ngozi. Donoa + ili kuifanya baridi (kuongeza kijani) na udonoe - ili kuifanya joto (ongeza nyekundu).
Ondoa Mand'yuma
Rekebisha wiani wa rangi ya mandharinyuma. Donoa + ili kuifanya ng’avu (nyeupe) na udonoe - ili kuifanya kolevu (nyeusi).
Pambizo ya Kufunga
Teua kama vile eneo la uunganishaji, kingo na mwelekeo wa nakala yako asili.
Pu. ili Itoshee Kar'i
Hunakili picha zilizotambazwa kwa ukubwa mdogo kuliko thamani ya Pung/Ong'a ili kutoshea ndani ya ukubwa wa karatasi. Iwapo thamani ya Pung/Ong'a ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi, huenda data ikachapishwa zaidi ya kingo za karatasi.
Ondoa Kivuli
Huondoa vivuli kwenye nakala asili inayoonekana kwenye nakala.
Fremu
Huondoa vivuli vinavyoonekana kwenye nakala unaponakili karatasi nene.
Katikati
Huondoa vivuli vinavyoonekana kwenye kituo cha nakala unaponakili kijitabu.
Ond. Mas'o ya Panchi
Huondoa mashino ya kufunga wakati wa kunakili.
Nakala ya Kadi ya ID
Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi.
Nakala ya Uthibitisho
Unapotengeneza nakala anuwai, unaweza kuanza kwa nakala moja ili kuangalia matokeo, na kisha kunakili mengine.
Futa rangi nyekundu
Teua ili kutoa nakala zenye vibambo vyekundu vilivyofutwa kwenye asili.